Kitchen Party Gala

Afya Yangu Kwanza...

Futa DELETE Kabisa Campaign

Ukipata Ujumbe Wowote Usiofaa...

Zig Zag Hot Stories

Tune on IDEA RADIO Fm 95.7 MHZ Arusha Tanzania......The Voice you Know, The Voice You Trust.

Zurii House of Beauty

Fashions ,Beauty ,Hairstyles.....

IMETOSHA Campaign

Tunawapenda Tutawalinda....

TUZO YA JAMII : PIGA KURA YAKO SASA


MUSWADA WA SHERIA YA MIAMALA YA KIELEKTRONIKI (ELECTRONIC TRANSANCTIONS) 2015.

30 Mar 2015

Maisha na Dini : Rais Kikwete Asema " Waislamu Anzisheni Mahakama ya Kadhi, Serikali Imegoma na Haitawaingilia"


Rais Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo. Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).
<<<<<<<<<<<<<<<< >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
RAIS Jakaya Kikwete amefafanua msimamo wa Serikali katika mjadala unaoendelea wa Mahakama ya Kadhi, na kuweka wazi kuwa Serikali haina mpango wa kuianzisha, wala kuiendesha.


Mbali na hiyo, Rais Kikwete ambaye jana alizungumza na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Dar es Salaam, pia alielezea kusikitishwa kwake na tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, lililowaelekeza waumini wao kupigia Katiba Inayopendekezwa kura ya Hapana.
Mahakama ya Kadhi
Akifafanua suala la Mahakama ya Kadhi, Rais Kikwete alisema Serikali ina msimamo wa mambo mawili katika mahakama hiyo.
Kwanza, alisema Serikali haina mpango wa kuianzisha na kuiweka katika Katiba na pili, haihusiki kuiendesha na badala yake, Waislamu wenyewe ndio watakaoiendesha.
Alisema kimsingi, mahakama hiyo ilikuwepo kabla ya Uhuru na kinachotakiwa kuzungumzwa ndani ya Bunge, ni Sheria ya Kutambua Uamuzi Unaofanywa na Kadhi.




Alifafanua zaidi kuwa Mahakama hiyo ya Kadhi, haihusiki na mambo ya jinai, isipokuwa mambo ya kijamii ikiwemo talaka, mirathi na mengine ya aina hiyo.
Alitoa mfano wa Sheria ya Kiislamu, iliyokuwepo tangu zamani, ambayo inatambua chombo hicho na kusisitiza kuwa kinazungumzwa, ni uamuzi unaofanywa na Kadhi utambulike tu.
Katika mfano huo, alisema Muislamu ukigombana na mke wake, kuna mabaraza ya usuluhishi ambayo huyo mwanamke atapaswa kwenda, ila wakishindwa na ataomba talaka ambayo inaidhinishwa na Kadhi, ambaye ndiye msajili wa vyeti vya ndoa kwa Waislmau.
Baada ya kutoa ufafanuzi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Shehe Alhad Musa, alimshukuru Rais Kikwete kwa ufafanuzi alioutoa na kusema Wakristo na Waislamu siku zote ni wamoja na wataendelea kuishi kwa amani, furaha na ushirikiano.
Katika hilo, Shehe Alhad alinukuu Biblia katika Kitabu cha Mathayo tano, mstari wa 25, ambao unasema; “Patana na mshitaki wako, mngali njiani, asije akakupeleka kwa Kadhi na Kadhi akakukabidhi kwa Polisi na Polisi akakutupa korokoroni.”
Katiba Pendekezwa
Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, ambayo inasubiri kupigiwa kura na wananchi, Rais Kikwete alisema Katiba hiyo imewakilisha vitu vingi kuliko Katiba iliyopo.
Alifafanua kwamba Katiba Inayopendekezwa, imeweka haki za makundi mbalimbali ya jamii, kuliko iliyopo na kuongeza kuwa yeye binafsi ameisoma na kurudia kuisoma, lakini hajaona mahali popote ambapo ina kasoro.
Alisema isingekuwa rahisi kuweka maoni ya kila mtu katika Katiba, na kufafanua kuwa yale ambayo hayajawekwa sasa hivi, utafika wakati wake na yatawekwa.
Alibainisha kuwa haikuwa rahisi kwa maoni ya kila mtu kuingia katika Katiba Inayopendekezwa, kwani hata CCM ilikuwa na mambo 60 waliyopendekeza, lakini kati ya hayo ni 12 tu yaliyoingia.
Rais Kikwete alisema Katiba sio Msahafu au Kurani, ambayo haiwezekani kubadilishwa hata nukta. Alitoa mfano wa Zanzibar, kwamba wakati kuunda Muungano, yapo mambo yalionekana ni muhimu kubakia katika Muungano, lakini kadri muda ulivyokwenda yameondoka.
Jukwaa la Wakristo
Akizungumzia tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, Rais Kikwete alisema amehuzunishwa na kufadhaishwa na tamko hilo la viongozi wa dini la kutaka waumini wao wajiandikishe kwa wingi, lakini wapige kura ya Hapana kwa Katiba Inayopendekezwa.
Tamko hilo lilitolewa na jukwaa hilo linaloundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT).
Rais Kikwete alisema, tamko hilo litakuwa pia limekwaza waumini, kwa kuwawekea mipaka ya kidemokrasia na kukwaza hata viongozi wenyewe.
Alitoa mfano kwamba kwa tamko hilo, muumini hataweza kusimama na kumwambia kiongozi wa dini asiwaingilie katika uamuzi, kwa kuwa kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila mtu, na ikitokea hivyo, hata kiongozi husika atakwazika.
Subira kwa NEC
Kuhusu uwezekano wa Kura ya Maoni kufanyika Aprili 30 kama ilivyotangazwa na Serikali, huku kazi ya kuandikisha wapigakura ikiendelea kusuasua, Rais Kikwete alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inayoratibu uandikishaji wa wapigakura, itazungumza kuhusu walipofikia wakati muafaka ukifika.
Amani
Kuhusu amani ya nchi, Rais Kikwete alisema viongozi wa dini pia wa jukumu kubwa la kuimarisha amani ya nchi.
Katika utekelezaji wa jukumu hilo, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao wajaribu kuepuka kutumiwa na watu wenye nia mbaya, kwa sababu wanafahamu kuwa viongozi wa dini wana ushawishi katika jamii na wana watu wengi nyuma yao.
Alisema machafuko yatakayotokana na mvurugano wa kidini, hakuna mtu atakayeweza kuyazuia, hivyo ni vyema viongozi hao waendeleze mshikamano.
Alitoa mwito kwa mikoa mingine nchini, kuunda kamati za amani kama ilivyo Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Dar es Salaam.

Madini Yetu :Kituo cha Jimolojia Kuwezesha Uongezaji Thamani Madini Nchini, Arusha

Mkandarasi wa kampuni ya Kiure Engineering iliyofanya Ukarabati Mkubwa katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) cha Jijini Arusha, Oswald Modu ( wa tatu kulia) akimkabithi funguo za vyumba mbalimbali vya kituo hicho, Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa tatu kushoto). Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Wafanyakazi wa kampuni ya Kiure Engineering.
Mratibu wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) Mussa Shanyangi (wa pili kulia), akiwaonesha Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Habari na Teknolojia Francis Fungameza namna mashine ya kukata mawe inavyofanya kazi.
Baadhi ya Wanafunzi katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) waki polish mawe wakati wa mafunzo. Wanafunzi hao wako katika mafunzo ya ukataji na unga’rishaji madini katika kituo hicho.
Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa Yahya (kushoto) akimweleza jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering Oswald Modu(wa tatu kulia) wakati wa ukaguzi wa jingo la kituo hicho kabla ya makabidhiano rasmi kufanywa.
Baadhi ya wanafunzi wa kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kilichopo Jijini Arusha. Wakiwa katika mafunzo ya kunga’risha madini. Kituo hicho kitawezesha shughuli za Uongezaji Thamani kufanyika chuoni hapo.
Sehemu ya Jengo la kituo cha Jimolojia Tanzania TGC, inavyoonekana pichani baada ya Ukarabati Mkubwa kufanywa na Kampuni ya Kiure Engineering. Jengo hilo limekabidhiwa rasmi kwa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa Yahya (katikati) na ujumbe wa Wizara na Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering wakikagua mfumo wa CCT katika kituo cha Jimolojia Tanzania. (TGC).
Baadhi ya Vinyango vilivyochongwa kwa madini yam awe katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC).
Na Asteria Muhozya, Arusha
Imeelezwa kuwa kukamilika kwa ukarabati  mkubwa wa kituo cha Jimolojia  Tanzania (TGC) cha Jijini Arusha ni mafanikio makubwa kwa Wizara ya Nishati na Madini hususan katika  tasnia  ya Uongezaji  Thamani  Madini nchini kwani  kitawezesha shughuli hizo kufanyika nchini.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini  (SMMRP) Idrisa   Yahya  mwishoni mwa wiki wakati wa makabidhiano ya kituo hicho  baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa  uliofanywa na kampuni ya  Kiure Engineering .
“Mkandarasi amejitahidi kufanya kazi katika muda tuliokubaliana na kazi imefanyika kama ilivyotakiwa. Hivi sasa tutautaja kama mradi uliokamilika”, alieleza Idrisa.
Aliongeza kuwa, mradi wa SMMRP utaendelea kukisaidia kituo   hicho ili kiweze  kutimiza malengo  yake  na kuhakikisha kinatoa taaluma katika masuala ya uongezaji thamani madini  na hivyo kuwezesha sekta ya madini  kuchangia zaidi  katika  pato la taifa. 
 Alisema kuwa, SMMRP imelenga katika kukiwezesha kituo hicho kuwa bora katika mafunzo ya uongezaji thamani madini nchini kutokana na umuhimu wa shughuli hizo kufanyika nchini badala ya madini hayo kusafirishwa nje ya nchi yakiwa ghafi.  

“Tumelenga katika kukiunganisha kituo hiki  na vyuo vingine duniani vinavyotoa taaluma katika masuala haya ili kupata uzoefu na kubadilishana taaluma.  Tunataka kituo hiki kifanye kazi iliyokusudiwa na kisimame peke yake hivyo lazima kiweke mipango mizuri.  Kwa upande wa wizara ina budi kutenga bajeti ya kituo hiki kiendelee   ili kutimiza malengo tunayoyatarajia”, alisisitiza Idrisa.
Kwa upande wake Mratibu wa kituo hicho Musa Shanyangi alisema kuwa, kituo hicho kinatarajia kuanza muhula mpya wa masomo ifikapo mwezi Juni mwaka huu katika fani za ukataji madini, masuala ya jimolojia, mafunzo ya usanifu na utengenezaji wa mapambo ya vito.
“Hivi sasa tunao wanafunzi 15 wanawake wanaosoma fani ya kukata na kung’arisha madini. Wanafunzi hawa walianza mafunzo tangu Novemba 2014 na wanasoma kwa ufadhili wa Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA)” alisema Shanyangi.
Aidha, Shanyangi aliishukuru Serikali kwa kutambua shughuli za uongezaji thamani madini nchini kwani zitaongeza wigo wa ajira, kipato cha mtu mmoja mmoja, kuwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi kupitia sekta hiyo ikiwemo pia  kuchangia katika pato la taifa.

Shughuli za uimarishaji na uendelezaji wa kituo hicho zinafanyika chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP). Kituo kitakuwa na maabara ya utambuzi wa madini ya vito, maktaba ya jimolojia na makumbusho ya madini ya vito.

Maisha Yetu : Ujamaa Intellectuals Network Watoa Msaada katika Kituo cha Kulelea Yatima cha Maunga Centre, Jijini DAR


 
 Mwasisi na Mratibu Mkuu wa Kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network Bw. Lusekelo Mwandemange akikabidhi msaada kwa Bi. Zainab Bakary Maunga wa kituo cha kulelea yatima cha Maunga Centre.
Bi. Mwajuma Njaritta  kutoka kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network akimkabidhi mmoja wa watoto Msaada wa vitabu kwa niaba ya watoto wengine katika kituo cha kulelea yatima cha Maunga Centre.
 
 Baadhi ya Misaada iliyotolewa na kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network
 Mwanzilishi na Mkuu wa kituo cha kulelea yatima cha Maunga kilichopo karibu na Kituo cha Polisi cha Hananasif  Kinondoni Bi. Zainab Bakari Maunga akitoa shukurani zake kwa kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network kwa kuleta misaada mbalimbali katika kituo hicho.
 
 Mwasisi na Mratibu Mkuu wa kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network Bw. Lusekelo Mwandemange akizungumza jambo wakati wa kutoa misaada hiyo na kuongeza kwamba huu ni mpango ambao wanaufanya kwa nchi nzima lengo ni kuwasaidia watu wasiojiweza, na pia ametoa ahadi ya kuendelea kutoa ushirikiano na kuendelea kusaidia zaidi kwa wale wasiojiweza.
 
 Katibu Mkuu wa Kituo cha kulela yatima cha Maunga akitoa neno la Shukurani baada ya kupokea misaada hiyo na kuwasihi watu wengine waguswe ili waweze kusaidia kama hawa walivyofanya
 Mmoja wa watoto akitoa Shukurani zake kwa niaba ya watoto wenzake baada ya kupokea Msaada huo.
 Baadhi ya watoto wakiwa pamoja na wanakundi wa Kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo

Teknolojia na Maisha : Wanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika maswala ya Computer kutoka Chuo cha Nelson Mandela walipokuwa Terrat, Simanjiro

 Na Laltaika Eliamani Laltaika - NM-AIST, Arusha

Celebrating Pioneer ICT education in rural Maasailand: Distinguished PhD Students in ICT from the Nelson Mandela African Institution of Science and Technology NM-AIST traveled to Terrat Village in Simanjiro over the weekend (Saturday 28th March) to congratulate 25 young Maasai men and women on completion of their Computer training course offered by the Terrat based Computer and Vocational Training Institute. It was humbling to be guest of honor at this historic moment./ Wanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika maswala ya Computer kutoka Chuo cha Nelson Mandela walipokuwa Terrat, Simanjiro mwishoni mwa wiki kuwapongeza wahitimu 25 wa kozi ya computer inayotolewa na chuo cha computa na ufundi stadi cha Terrat. Kwa unyenyekevu mkubwa nilikuwa mgeni rasmi katika hafla hii ya kihistoria.

With retired District Commissioner James K. Millya (left) and DC for Kankonko, Kigoma Hon. Peter Toima
 Speech by the Guest of Honor/Hotuba ya mgeni rasmi : Laltaika Eliamani Laltaika
 Academic Procession/Msafara wa kitaaluma
 Representative of NM-AIST/Mwakilishi wa Nelson Mandela
 Inspiration unlimited, Scientist from Mandela/Mwanasayansi kutoka Nelson Mandela akiwapa hamasa wahitimu
 President of the NM-Women Association in Science, Technology, Engineering and Mathematics NM-WASTEM
 Parents and other invitees/Wazazi na wahitimu wengine
 Celebratation/Shamra shamra
Group photo/picha ya pamoja

Matukio : Dkt. Gharib Bilal Afunga Kongamano la 3 la Vijana wa Tanzania na China, Jijini Arusha


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China kuhusu masuala ya Uongozi, wakati alipokuwa akiwasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto kufunga kongamano hilo jana Machi 29, 2015.
Meza kuu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake jana Machi 29, 2015 wakati akifunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika, Chen Lin, baada ya Makamu kufunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka ukumbini hapo baada ya kufunga rasmi Kongamano la tatu ya Viajana wa Tanzania na China, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka ukumbini hapo baada ya kufunga rasmi Kongamano la tatu ya Viajana wa Tanzania na China, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimksikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifunga rasmi Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimksikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifunga rasmi Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimksikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifunga rasmi Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimksikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifunga rasmi Kongamano hilo.
 Picha na OMR

Maisha Yetu : Benki ya NBC yatoa Msaada wa Mafuta, Kofia, Pikipiki na Kompyuta kwa Albino


Mkuu Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mussa Jallow (wa tano kulia) akikabidhi msaada wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, kompyuta, kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Ofisa Mkaguzi wa Sheria za Ndani za Benki wa NBC, Lilian Kawa (katikati) akikabidhi msaada wa kofia kwa Katibu wa Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Aicha Joakim Ngure (wa tatu kushoto) katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta na mafuta maalumu ya ngozi ili kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na tatizo unaotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mafuta maalumu ya ngozi kwa mmoja wa wawakilishi kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta na kofia vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Meneja Udhibiti wa Sheria wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanakombo Joshua (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa kampyuta kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki , kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Ofisa Uchunguzi wa Idara ya Udhibiti wa Sheria wa Benki ya NBC, Mathias Raymond (wa pili kulia) akikabidhi msaada kompyuta kwa mmoja wa wawakilishi kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kofia na mafuta ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Sheria wa NBC, Joyce Mbago (wa tatu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni 3.2 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa pikipiki , kofia, kompyuta na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC, wakiwa na wawakilishi wa Chama cha Albino Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla hiyo.

Matukio : Tume ya Mipango Yapongezwa Kwa Ufanisi



Na Mwandishi Wetu, Adili Mhina 

Ofisi ya Rais, tume ya mipango imepongezwa kwa hatua kubwa iliyopiga katika kutekeleza majukumu mbalimbli ya kitaifa.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango lililofanyikia mjini Kibaha mwishoni mwa juma.
Mheshimiwa Ndikilo alieleza kuwa Tume ya mipango imepiga hatua kubwa katika kutekeleza majukumu yake ambayo ni pamoja na kutayarisha mpango wa taifa wa kila mwaka, kusambaza machapisho mbalimbali ya Tume ya Mipango, Kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa, na kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano (2011/12-2015/16).
Pamoja na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu ya Tume, Mkuu wa Mkoa alieleza kufurahishwa kwake na ufanisi wa viongozi pamoja na watumishi wa Tume ya Mipango kwa kuandaa mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma, “ninaipongeza tume ya mipango kwa kundaa mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma (Public Investment Management Manual), pamoja na kukamilisha tafiti mbalimbali zinazoharakisha mendeleo ya uchumi wa nchi yetu na mahitaji ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Mendeleo 2025.”
Vilevile uongozi wa Tume ya mipango umepongezwa kwa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wake wa kada mbalimbali kwa kuwapeleka mfunzo ya muda mrefu na mfupi, semina na warsha zinazofanyika ndani na nje ya nchi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.
Aidha Mheshimiwa Ndikilo amesisitiza wajumbe wa baraza hilo kuwaelimisha watumishi wenzao juu ya  umuhimu wa kila mfanyakazi kutimiza wajibu wake katika sehemu ya kazi ili kufikia malengo ya pamoja baina ya mwajiri na watumishi.
“Pamoja na mambo mengine Baraza linawajibu wa kuishauri Tume kwa lengo la kuleta tija na mshikamano baina ya mtumishi na mwajiri, si jambo la busara kwa watumishi kutumia muda mwingi katika kudai maslahi zaidi kuliko kupima kiwango cha utekelezaji wa wajibu wao,” alisisitiza mhandisi Ndikilo.
Awali, Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, alieleza kuwa katika mkutano huo wajumbe watapata fursa kujadili mada nne amabazo ni mpango wa makisio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2015/16, Elimu ya jinsia mahala pa kazi, utekelezaji wa sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013, na haki na wajibu wa mwajiriwa mahala pa kazi. Lengo la mada hizo ni kutoa fursa kwa watumishi kujifunza zaidi ili kuweza kuboresha utendaji wao wa kazi ili kufikia lengo la Tume ya mipango la kukuza uchumi wa Taifa.
Mkutano huo wa siku mbili unaozingatia mwongozo wa Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Baraza hilo limehudhuriwa na wakuu wote wa Klasta, Idara na vitengo, wajumbe wa TUGHE Taifa, TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Halmashauri ya TUGHE tawi la Tume ya Mipango, pamoja na mjumbe mmoja mmoja kutoka klasta, Idara na Vitengo.


 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akihutubia wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, ambapo alionesha kuridhishwa na viongozi na wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwa weledi wao katika kutekeleza majukumu ya Taifa.
 Picha ya Pamoja ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya Raisi, Tume ya Mipango wakiwa pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
 Mjumbe Zena Hussein akijadili mada katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi. Wa kwanza kulia (mwenye shati ya mikono mirefu) ni Bw. Omary Abdallah ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mipango na Usimamizi, akifuatiwa na Bw.  Dunstan Nyeme ambaye pia ni Kaimu Mhasibu mkuu, na kulia ni mjumbe  Bw. S. Fisoo.
 Mjumbe wa baraza bibi Mary Mwangisa, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, akichangia mjadala wakati wa majadiliano ya wajumbe ndani ya mkutano.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa wanafuatilia kwa makini mada zinazotolewa wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakati mjini kibaha.

Marafiki

Blogu za Muziki