MADIWANI WA CHADEMA WAPIGWA: NAIBU MEYA MHE. PROSPER MSOFE NA EPHATA NANYARO WAPIGWA NA ASKARI WA JIJI LA ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


16 Apr 2014

MADIWANI WA CHADEMA WAPIGWA: NAIBU MEYA MHE. PROSPER MSOFE NA EPHATA NANYARO WAPIGWA NA ASKARI WA JIJI LA ARUSHA

Mh. Naibu Meya Prosper Msoffe akiwa na Mh. Ephata Nanyaro Diwani wa Levolosi, wote kwa pamoja wakishikilia kadi zao za matibabu kwenye Kituo cha Afya cha Levolosi, Wamepigwa na Mgambo wa Jiji kwasababu ya kutetea Uonevu na Udhalilishaji Unaofanywa na Migambo wa Jiji

Na mwandi wetu, Arusha

Naibu meya wa  halmashauri ya jiji la  Arusha Prosper Msofe pamoja na diwani wa kata ya kaloleni leo wamechezea kichapo   kikali kilichowapelekea majeraha makali kutoka kwa  mgambo   wa jiji  la Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari diwani wa kata ya Kaloleni Ephata  Nanyaro alisema kuwa  tukio hilo  la wao kupigwa limetokea majira ya asubui  katika depoti  ya manispaa ya jiji  wakati walipoamua kwenda katika eneo hilo mara baada ya kusikia wananchi  ambao ni wamachinga wakiwemo wamama wamekamatwa na kupelekwa katika  depoti hiyo ya manispaa ya jiji  huku wakiwa wanapigwa.
  Diwani huyo alisema kuea  naibu meya ameweza kupigwa sehemu mbalimbali za mwili ikiweo miguuu ambapo kwa upande wake  yeye amueumizwa maeneo ya goti lake la kushoto ,mdomo  pamoja na taya yake ya kushoto .

Aidha alibainisha kuwa wao kama madiwani walipewa taarifa  leo asubui  kuwa kuna wananchi waliopo soko kuu wanapigwa na askari mgambo wa jiji bila sababu yeyoyote  ,huku akibainisha kuwa kisheria  mgambo ao  walikuwa hawatendi haki kwa jinsi waivyokuwa wanakamata watu   kwani walikuwa hawafati  sheria   ya nchi ,bali walikuwa wanaenda kinyume na kanuni ya katiba ya nchi inasema usimpige mtu mara baada ya kumkamata bali umfikishe katika mikono ya sheria  ikiwemo polisi.


Akielezea maelezo ya awali naibu meya Prosper Msofe alisema kuwa wao walipewa taarifa  kutoka kwa baadhi ya wafanya biahara wadogo wadogo kuwa wanakamatwa na kupigwa  pasipo sababu  na vitu vyao vinachukuliwa hivyo ndipo walipoamua kuwafata mgombo hao katika depoti yao na walivyofika yeye kama naibu meya aliamua kuwaambia mgambo wale kwanini mnawapiga wananchi bure na sheria hairuhusu kupiga mtu bali kumkamata  ndipo magambo wale waliwageuzia kibao na kuanza kuwapiga wao.

“sisi tulivyofika pale niliamua kuwauliza vizuri mgambo wale kwanini mnawapiga wananchi mara baada ya kuwakamata badala ya kuwachukulia sheria ya kuwapeleka polisi na sio kuwaweka huku depo  basi mgambao wale ambao waikuwa zaidi ya  15 hawakuongea kitu bali walituambaia tu nyie ndo mnajidai madiwani wenyeviere here na kuwamua  kuanza kutushambulia”alisema msofe
Alisema kuwa kufuataia tatizo hilo la wanachi kupigwa mara kwa mara  mpaka sasa wananchi zaidi ya watatu wameshavunjwa miguu huku wengine zaidi ya sitini wameshapigwa favu na viboko na kati yao ,kunabaadhi yao ambao wame lazwa katika hospitali ya mkoa ya mounti meru wakiwa wanatibiwa  na halmashauri  ambapo alibainisha kuwa pia wananchi hao waliopigwa na kulazwa pindi watakapo pon a wanampango wa kuwafikisha mgambo hao mahakamani kusiana na matukio hayo ya kuwapiga.

Akiongelea tukio hilo meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo  alisema kuwa wao kama madiwani na meya wa jiji amepokea kwa masikitiko makubwa  tukio hilo na alibainisha kuwa walichofanya mgambo hao wamekiuka sheria bali alisema kuwa wamekaa kikao cha muda na wameamua kuwasimamisha kazi mgambo wote kwa kitendo cha kuwazalilisha madiwani hao .

Alibainisha kuwa  katika kipindi hicho ambacho madiwani hao wamesimamishwa kazi wataunda kamati ya uchunguzi ambao itawashirikisha baadhi ya madiwani pamoja na watendaji wa halimashauri  ili kujua na ni anamakosa kati ya madiwani na mgambo na iwapo itagundulika ni mgambo basi watawachukuli hatua za kisheria.


Wakimweleza Mwandishi wa Habari kuwa tumepigwa na Mgambo wa Jiji kwasababu ya kutetea Uonevu na Udhalilishaji Unaofanywa na Migambo yoa wa Jiji kwa wananchi na wafanyabiashara ndogondogo.

Siamini kama Wafanyakazi wangu wanaweza nishambulia kiasi hili

Mh Kessy Diwani wa Kaloleni alikuwepo kuwapa joto madiwani wenzake

Chriss akiongoza Makamanda kusubiri mpaka kieleweke

Tutakomaa hapa Mpaka kieleweke

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad