TANZANIA TUNAWEZA :UBUNIFU MKUBWA IRINGA GARI LA MBAO LAWAVUTIA WENGI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Apr 2014

TANZANIA TUNAWEZA :UBUNIFU MKUBWA IRINGA GARI LA MBAO LAWAVUTIA WENGI


Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao

Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha umadhubuti wa bori lake

Mwanahabari huyu Oliva Moto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubunifu huo.
HUWEZI KUAMINI, lakini huo ndio ukweli. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine.

Gari hili linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, Kenny Mwangoka.

Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika vibaya.

Jitihada za Mwangoka kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.

"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema.

Anasema baada ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.

"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema.

Anasema gari hilo atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti. Na Francis Godwin wa Matukio Daima

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad