TOKOMEZA UJANGILI :WAZIRI NYALANDU AZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA KUKAMATWA KWA MAJANGILI 6 NA MENO YA TEMBO 53 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


1 Apr 2014

TOKOMEZA UJANGILI :WAZIRI NYALANDU AZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA KUKAMATWA KWA MAJANGILI 6 NA MENO YA TEMBO 53

DSCF3201

Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha juu ya kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7 na majangili sita
DSCF3202Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Sheluteteakifurahia jambo na wanahabari jijini Arusha
DSCF3199
DSCF3198Wanahabari wa vyombo mbalimbali wakifatilia jambo kutoka kwa Waziri wa maliasili na utalii

Wizara ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu pamoja na majangili sita katika wilaya ya manyoni mkoani Singida
 
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo
 
Waziri Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu
 
Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili, serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana
 
Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasaka wauwaji wa tembe 26,huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyamapori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama
 
Pia alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyamapori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo. Na Pamela Mollel wa Jamii Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad