WANAWAKE NI NGUZO YA TAIFA :MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHIWA CHETI CHA ULEZI WA HIARI WA CHAMA CHA WENZA WA MABALOZI WA AFRIKA WALIOKO UBELGIJI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Apr 2014

WANAWAKE NI NGUZO YA TAIFA :MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHIWA CHETI CHA ULEZI WA HIARI WA CHAMA CHA WENZA WA MABALOZI WA AFRIKA WALIOKO UBELGIJI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma akipokewa na ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa siku mbili baina ya Afrika na Ulaya mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Sheraton huko Brussels nchini Ubelgiji akitokea nchini Uingereza tarehe 2.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Ubelgiji.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Madagascar Mama Lalao Rajaonarimampianina muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa Afrika kwa ajili ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa Afrika na Ulaya unaofanyika huko Brussels.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadaye wakibadiishana mawazo na Mke wa Rais wa Congo Mama Antoinnethe Sassou Nguesso wakati wa hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Jumuia ya wenza wa mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao huko Ubelgiji.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Cameroon Mama Chantal Biya muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye chakula cha mchana walichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao huko Ubelgiji kwenye hoteli ya Sheraton.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea cheti maalum cha ulezi wa heshima wa Chama cha wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika walioko nchini Ubelgiji (Honory Patronese of the Association of the Spouses of African Ambassadors in Belgium) kutoka kwa Mke wa Balozi wa Cameroon nchini Ubelgiji Mama Christiane Eloundov de Evina wakati wa chakula cha mchana walichowaandalia wake wa Marais wa Afrika jijini Brussels.
Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mama Adelaida Kamala akimkabidhi Cheti Maalum cha ulezi wa heshima cha wenza wa mabalozi wa Afrika walioko Ubelgiji, Mke wa Rais wa Cameroon Mama Chantal Biya wakati wa chakula cha mchana walichowaandalia wageni hao kwenye hoteli ya Sheraton.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika pamoja wa wenza wa Mabalozi wa nchi hizo mara baada ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenza hao tarehe 2.4.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad