ANGELLA BONDO SHOW : Kutana na Hasheem 'Ramsey' Kambi akielezea undani wa maisha yake binafsi na sanaa kiujumla - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Jul 2014

ANGELLA BONDO SHOW : Kutana na Hasheem 'Ramsey' Kambi akielezea undani wa maisha yake binafsi na sanaa kiujumla



Hasheem 'Ramsey' Kambi ni mmoja kati ya wasanii maarufu wa filamu nchini Tanzania. Ana historia nzuri ya kua mchezaji wa mpira wa miguu lakini baadae  alijikuta akiingia kwenye sanaa ya maigizo.
Ameshacheza filamu zaidi ya mia moja mpaka sasa na kwa ujio wake mpya katika kukuza wigo wa soko lake ameamua kuvuka mipaka kushirikiana na wasanii wa Nigeria na Ghana ambao soko lao ni kubwa zaidi Africa. Binafsi anavutiwa zaidi na uigizaji wa Pete Edoche wa Nigeria ambae ndiye Role Model wake. Na kwa Ghana anavutiwa zaidi na kazi za Majid na John Dumelo. Na katika filamu yake mpya inatakayoingia sokoni siku chache zijazo amemshirikisha 'Vanvica' kutoka Ghana Na pia yuko njiani kumkaribishisha nchini Tanzania msanii kutoka Nigeria Pete Edochie kwa kazi zaidi za filamu ikiwa ni kupanua zaidi wigo wa soko pamoja na kujenga uhusiano mzuri pamoja na wasanii wa nchi nyingine Africa. 
Hasheem Kambi ameongea mengi kuhusuana na mabadiliko ya kisanaa ikiwemo uigizaji wa wasanii wapya na wa zamani na pia kuhusu changamoto kubwa wanazokutana nazo ikiwemo soko la kazi zao.

Usikose kutazama kipindi hiki cha THE ANGELLA BONDO SHOW ili eweze kumfahamu Hasheem Kambi kiundani na pia sanaa ya filamu kwa ujumla. Kipindi hiki kitakua kinaruka hewani kupitia vituo viwili vya Television vitakavyotajwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad