DINI ZETU : DKT. GHARIB BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA QUR-AN JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Jul 2014

DINI ZETU : DKT. GHARIB BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA QUR-AN JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Hatham Sadar, kutoka nchini Kenya wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu na majaji wa mashindano hayo baada ya zoezi la kukabidhi zawadi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad