MAPISHI, Na Chef Kile :Nyama ya Kuponda na Kuchoma Pamoja na BBQ Souse - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Jul 2014

MAPISHI, Na Chef Kile :Nyama ya Kuponda na Kuchoma Pamoja na BBQ Souse





Naam tuone jinsi ya kuandaaa nyama ya kuponda na kuichoma; na kutengeneza souse kwa kutumia BBQ Spiced and smoked souse.

MAHITAJI
  • Nyama ya ng’ombe mnofu ( steak meat) nusu kilo (1/2)
  • Pilipili Manga
  • Chumvi
  • BBQ souse (smoked and spiced) vijiko 4 vya mezani
  • Vitunguu swaumu punje 5
  • Vitunguu maji  viwili
  • Pili pili hoho 2
  • Limao moja
JINSI YA KUANDAA NA KUCHOMA NYAMA
nyama ya kuponga na kuichoma
Kwanza kabisa washa oven yako kabisa kama utachoma kwa oven au andaa moto kama utachoma kwa njia ya mkaa. Kisha ile nyama yako ikate mara mbili kwa staili ya ubapa hivi. Kisha iponde ponde hadi ilainike kabisa. Sasa weka chombo aina ya frying pan kwa moto na weka mafuta kidogo sana wacha ikiwa inapata moto.
Sasa ili nyama yako iwekee viungo aina mbili tu kwa sasa – ipakae pili pili manga na chumvi pande zote mbili. Kisha ziweke katika frying pan kwa ubapa …. lengo hapa ni kupata ule mkauko wa kama nyama ya kurosti… hivyo kama upande mmoja ukiwa umekauka vema basi geuza ili uweze kupata makauko sawa upande zote.
Baada ya hapo zitoe hizo nyama na uendelee kuzichoma kwa oven au jiko ambalo umeamua kutumia. Ila ile frying pan iache kwenye moto kwani sasa wakati nyama inaiva tutatengeneza ile souse ya kula na hiyo nyama.
SASA KUTENGENEZA BBQ SOUSE
Kwenye hicho chombo unaweza ongeza mafuta ka yaliopo waona hayatoshi, kisha weka vitunguu na endelea kuvikaanga na uweke vile vitunguu swaumu, pilipili manga, chumvi kidogo , mixed herb kisha endelea kuviunga hadi viwe kama vinaelekea kuiva na kubadili rangi kidogo – kama vinashika chini unaweza wema maji moto kidogo tu ….. Kisha weka ile BBQ souse (Angalia video kwa maelezo zaidi) , endele kuikoroga kidogo kisha kamulia lile limao moja ….kwa kumalizia unaweza weka majani ya giligilani na itakuwa tayari.
nyama ya kuponda na kuchoma pamoja na bbq souse
Sasa kama nyama yako waona iko tiari kule unakoichoma ndio muda wa kuikatakata na kuweka kwenye sahani alafu ile souse ndio unaweka juu ya hiyo nyama tayari kwa kufurahia mapishi yako.

Kwa maswali na majibu ya hapo kwa hapo ; piga simu +255 654 088 500

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad