MATUKIO, MAISHA : KAMPUNI YA AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA, JIJINI MWANZA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Jul 2014

MATUKIO, MAISHA : KAMPUNI YA AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA, JIJINI MWANZA

Mafuta kwa  Kituo.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na wadau wa Airtel. 
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda" Kauli ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema.
Twaha bin Bakari Utari ambaye ni Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  ambao ni wamiliki na kituo  ameshukuru kwa msaada huo toka Aitel huku akihamasisha wadau wengine kuiga mfano huo kwa ustawi wa jamii ya Watanzania. 
Sambamba na kuzibainisha changamoto wanazokabiliana nazo kama vitabu, madaftari,magodoro na sehemu za kulala,  msimamizi wa kituo Al-Hajji Hussein pia naye alikuwa na yake ya kusema. 
 
Ahmad Mustapha ni mmoja kati ya vijana wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake.
 
Shumbana Hassan ni mmoja kati ya watoto wa kike wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake. 
 
Kampuni ya simu  za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari katika vituo vinavyolea watoto waliopo katika mazingira magumu nchini.

 Kupitia mpango  huu Airtel  imetoa msaada wa chakula kwa kituo cha Sharif Saidi Al-Bath kinacholea watoto yatima kilichopo Nyegezi Majengo Mapya Jijini Mwanza

  Akiongea wakati wa kukabithi msaada huu , Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana Raphael Daudi alisema”   Airtel Kwa kutambua changamoto nyingi zinazozikumba jamii tumeonelea ni vyema katika mfungo huu wa ramadhani kutenga muda wa kutembelea na kutoa msaada kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini. Leo tumetembelea kituo hiki cha Sharif Saidi Al-Bathi na kuwapatia msaada wa chakula ambacho kitawasaidi hata baada ya mwezi wa ramadhani.

 lengo letu ni kuhakikisha tunagusa mahitaji ya jamii kwa ujumla, husasani watoto kupitia vituo vinavyowatunza huku tukihakikisha tunarudisha faida tunayoipata kwa kuwafikia watanzania wengi kupitia shughuli zetu za huduma kwa jamii kila mwaka. 

Kwa upande wake  Kiongozi wa Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath bwana Alhaji Hussein Mussa  Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu, tumefurahi sana na kuona kumbe watanzania wenzetu na mashirika mbalimbali wanaunga mkono jitihada zetu katika kuhakikisha tunawalea na kuwasomesha watoto yatima. Kituo chetu bado kina mahitaji mengi hivyo natoa wito kwa taasisi zingine  kujiunga na kuendelea kusaidia kituo chetu na vituo vingine nchini

 Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo hiki wameishukuru Kampuni ya Airtel kwa msaada wa vitu mbalimbali walivyotoa na kuyatala makampuni mengine kuiga yale yaliyofanywa na kampuni hiyo.

 Vituo vingine vitakavyopata msaada kutoka Airtel  ni pamoja na  New Hope Family group-Temeke, Al-Hidaya children’s Home-ilala, Irishad  Madrasah-Mbezi kwa Msuguri (kinondoni), Kiboa orphanage-Arusha  na Heartfelt orphanage care Mbeya

 Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath chenye  watoto Yatima zaidi ya 50 kilichopo Mwanza tayari kimepokea msaada kutoka Airtel mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad