MICHEZO : NAIBU WAZIRI MHE. JUMA NKAMIA AZINDUA RASMI KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA" KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Jul 2014

MICHEZO : NAIBU WAZIRI MHE. JUMA NKAMIA AZINDUA RASMI KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA" KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA

 Mwina kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Zawadi yake ya Kitabu.
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Collin Frisch akiwa na Mtunzi wa kitabu cha Historia ya Simba Mwina Kaduguda kwenye uzinduzi Rasmi wa kitabu hicho kwenye ukumbi wa Klabu ya Simba
 Wageni waalikwa waliokuja Kushuhudia Uzinduzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Kutoka kulia ni Fredrick Mwakalebela,Said Tulliy(Mjumbe wa kamati ya Utendaji),Hassan Dalali(mwenyekiti Mstaafu) na Mtunzi wa kitabu Hicho Mwina Kaduguda
 Wapenzi,wanachama wa Simba Pamoja na Vyombo vya habari waliohudhuria Uzinduzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" wakifuatilia kwa makini Uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya  Akielezea namna walivyochapa kitabu hicho na ubora wake .
 Mjumbe wa kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Bwana Collin Frisch akiongea kwa niaba ya Rais wa Simba,ambapo amempongeza sana Mwina Kaduguda na kusema ameiweka Klabu ya Simba kwenye Kumbukumbu muhimu sana kwenye soka la Tanzania hivyo inatakiwa aungwe mkono kwa nguvu zote.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akitoa neno kumpongeza Mwina Kaduguda  kwa kufikiria mbali sana kwa kuweka soka la Tanzania kwenye maandishi namna klabu ya simba ilivyoanza,Akaongeza kuwa Klabu za soka Tanzania zinatakiwa kuwa na watu kama Mwina Kaduguda ili kuleta maendeleo ya soka.Naibu waziri pia akasisitiza ni wakati wa kila mwanachama kujituma kwa bidii na kuacha kukaaa kwenye korido za Klabu na kupiga Zoga.
Mwina kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Zawadi ya Kitabu ambayo ameomba apelekewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete.


 Mwina Kaduguda Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" akielezea kwa kina Magumu gani amepitia wakati anaanza kuandaa kitabu hicho,Wa kwanza Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia na Katikati ni Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho.Akielezea kwa ufupi Mwina Kaduguda amesema kwamba Dhumuni kubwa la Kutunga kitabu hicho ni kutaka kutunza historia ya soka ya Timu hiyo isipoteee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad