UCHUMI WETU : DKT. JAKAYA KIKWETE AVUKA MTO PANGANI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Jul 2014

UCHUMI WETU : DKT. JAKAYA KIKWETE AVUKA MTO PANGANI


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiangalia mandhari ya mji wa Pangani wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.Sehemu kubwa ya mji huo imo katika hatari ya kumezwa na bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali imeahidi kujenga ukuta pembezoni mwa mto Pangani ili kuzuia athari za kimazingira kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya hotuba zake akiwa ndani ya kivuko kipya cha MV Pangani II wakati akivuka mto Pangani kutoka Tarafa ya Bweni kuelekea Pangani mjini wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Pangani (Jumamosi).Rais Kikwete ambaye alikuwa mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya wiki moja alihitimisha ziara hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa serikali itajenga kivuko kingine kwenye mto huo chenye uwezo mkubwa zaidi ili kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii wilayani humo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya majumuisho wakati akihitisha ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Tanga ambapo alizindua na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad