WAKUTWA NA MABOMU : WAWILI WAKUTWA NA MABOMU 7 YA KUTUPWA KWA MKONO, SOMBETINI ,JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


22 Jul 2014

WAKUTWA NA MABOMU : WAWILI WAKUTWA NA MABOMU 7 YA KUTUPWA KWA MKONO, SOMBETINI ,JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI)Isaya Mngulu akishauriana na maafisa wake leo


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA 


                    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha,  ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni:
1.  SHAABAN  MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26  Kabila,  Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
2.  ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
3.  MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
4.  JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
5.  ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji  Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
6.   SAIDI MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku   maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja. Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.


………………...…………..
ISAYA MNGULU-CP
MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad