AFYA YETU : BODI YA DAWASA YATEMBELEA MIRADI YA MAJI YA RUVU CHINI NA RUVU JUU - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Aug 2014

AFYA YETU : BODI YA DAWASA YATEMBELEA MIRADI YA MAJI YA RUVU CHINI NA RUVU JUU

 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Alhaji Said El-Maamry (kushoto) akiuliza jambo kwa Meneja Miradi wa DAWASA,Ing. Romanus Mwang'ngo (kulia) juu ya Mtambo wa Ruvu chini,wakati wa ziara yao iliyofanyika leo Agosti 20,2014.Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dkt. Eve-Hawa Sinare
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa pili kushoto) akijadiliana jambo na Makamu wake,Alhaji Said El-Maamry (kulia) mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea miradi ya Ruvu Juu na Ruvu chini leo Agosti 20,2014.Wengine pichani ni Wajumbe wa Bodi hiyo,Bw. Daniel Machemba (kushoto) na Ing. Mary Mbowe (wa pili kulia)
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yao katika Miradi ya Ruvu Juu na Ruvu chini.
 
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Ing. Archerd Mutalemwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna Shirika lake lilivyojipanga kuwaondolea kabisha hadha ya maji Wakazi wa Jijini la Dar es Salaam wakati akielezea kukamilika kwa Mtambo wa Maji wa Ruvu chini wenye Uwezo wa kutoa maji Lita Milioni 270 kwa siku ukitofautisha na uwezo wa Mtambo wa zamani uliokuwa ukitoa lita chache. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yake hiyo aliyoambatana na Wajumbe wake wote.
 Mhandishi Mshauri wa Kampuni ya UWP,Chacha Wambura (mwenye kizibao cha rangi ya chungwa) akitoa maelezo ya Maendeleo ya Mradi wa Ruvu chini kwa Ujumbe wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) uliotembelea Mradi huo Agosti 2014.
 Sehemu ya Mabomba ya kusafirishia Maji katika Mtambo wa Ruvu chini.
  Mhandishi Mshauri wa Kampuni ya UWP,Chacha Wambura akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare wakati wakitembelea sehemu ya Mtambo wa Maji wa Ruvu chini uliomalizika matengenezo yake.
Sehemu ya visima vya Maji Ruvu chini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad