TOKOMEZA UKATILI KWA WANAWAKE :MBEPAU YAZINDUA MRADI KUHUSU KUZUIA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE MBEYA VIJIJINI. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Aug 2014

TOKOMEZA UKATILI KWA WANAWAKE :MBEPAU YAZINDUA MRADI KUHUSU KUZUIA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE MBEYA VIJIJINI.

  Mkurugenzi wa MBEPAU, Jane Lawa, akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 Mjumbe wa bodi ya MBEPAU, Philimon Mwansasu, akimkaribisha mgeni rasmi, wakati wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 Mgeni rasmi,Afisa Tarafa ya Usongwe, Felix Lyaniva, akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya kutambulisha mradi wakifuatilia kwa makini.
Picha ya pamoja baada ya semina.
 
KITUO cha Msaada wa kisheria kwa wanawake(MBEPAU) kimezindua mradi mpya kuhusu kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wanawake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 
Utambulisho wa mradi huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Royal Tughimbe uliopo Mbalizi na kuwashirikisha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ambao ni viongozi wa dini, watendaji wa Kata, viongozi na mila na watu mashuhuri.
 
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika utambulisho huo, Mkurugenzi wa MBEPAU, Jane Lawa, alisema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ilikuwa ni kuwasadia wanawake na watoto katika sheria zinazowabagua na kuwakandamiza.
 
Alisema pia kupitia MBEPAU wanawake na watoto wanaweza kuzitambua sheria na kuzilinda na kuzitetea haki zao baada ya kuzifahamu na kuzitambua.
 
Aliongeza kuwa hayo yote yametokana na gharama kubwa ya Wanasheria katika kushughulikia malalamiko yanayopelekwa wanawake wengi wasiojiweza na utaratibu wa kutoza fedha kabla ya huduma ufanywao na wanasheria.
 
Mama Lawa alisema katika Mradi huo mpya chini ya ufadhili wa Legal Services Facility(LSF) ya nchini Denmark utafanyika kwa miezi 30 kwa gharama ya shilingi Milioni 200.
 
Alisema malengo ya Mradi ni kuongeza ufikiaji wa huduma za kisheria kwa wanawake na wanaume wilayani Mbeya, kuwajasirisha  wanawake kuweza kutumia mifumo ya kulinda haki zao na kuongeza mwitikio wa jamii katika kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani Mbeya.
 
Alisema kutokana na mradi huo wasaidizi wa kisheria 50 wamepata mafunzo juu ya ulinzi wa haki za wanawake na utoaji wa huduma za kisheria kwa Halmashauri za wilaya Mbeya na Jiji.
 
Aliongeza kuwa viongozi 50 wa jadi, kisiasa na dini pia wamepata mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na utambulisho wa mradi kwa wadau 80 kutoka Halmashauri ya wilaya Mbeya na Jiji.
 
Awali akizindua mradi huo, Mgeni rasmi wa tukio hilo, Katibu Tarafa wa tarafa ya Usongwe, Felix Lyaniva, alilipongeza Shirika la MBEPAU kwa juhudi zao za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa kipaumbele kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
 
Alisema ili juhudi hizo ziendelee kuungwa mkono ni vema washiriki wa Semina hiyo wakafikisha elimu kwa wananchi katika ngazi za chini ili wawe na uelewa juu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na msaada wa kisheria.
 
Aidha alitoa wito kwa Wamiliki wa Asasi za kiraia kufikisha huduma zao vijijini kwa kuwa wanaowalenga zaidi ni wanawake na watoto waishio vijijini hivyo ni bora kujenga ofisi huko huko kuliko kujikita mijini tu.

Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad