TUWATUMIKIE WANANCHI :RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA KISIMA CHA MAJI, LAMBO KATIKA KIJIJI CHA JAMII YA WAFUGAJI CHA MBALA,CHALINZE - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Aug 2014

TUWATUMIKIE WANANCHI :RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA KISIMA CHA MAJI, LAMBO KATIKA KIJIJI CHA JAMII YA WAFUGAJI CHA MBALA,CHALINZE


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akionozana na akina mama wa jamii ya kimasai waliobeba maji waliyoyateka baada ya mbunge huyo kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani jana. Kisima hicho pamoja na lambo la kunyweshea mifugo vimejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. Kushoto ni Kiongozi wa mradi huo, Joseph Chagama na nyuma yake ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana.
 Ridhiwani Kikwete akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho. Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana.
 Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua kisima hicho.
 Ridhiwani Kikwete akifungua maji ikiwa ni ishara ya kuzindua lambo la kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Mbala kinachokaliwa kwa asilimia kubwa na jamii ya wafugaji
 Ng'ombe wakitoka kunywa maji kwenye lambo hilo
 Watoto wa kimasai waonja maji ya kwenye lambo baada ya uzinduzi
 Kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Wasabato la Mbala, ikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, mkoani Pwani jana. Kanisa hilo limejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. 
 Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia) akishiriki katika maombezi
Kwaya ya Kanisa la Wasabato la Manzese wakimwimbia bwana wakati wa hafla hiyo. . PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad