UCHUMI NA BIASHARA :Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) zatiliana saini kukuza biashara - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.

Post Top Ad

18 Aug 2014

UCHUMI NA BIASHARA :Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) zatiliana saini kukuza biashara

1(16)
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL), leo mchana, makubaliano hayo yataziwezesha pande hizo mbili kushirikiana kibiashara ambapo USL itapewa kipaumbele kwenye kupanga katika miradi ya ujenzi ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa popote nchini.
2
Meneja Mkuu wa Uchumi Supermarkets Tanzania, Chriss Lenana akifafanua Jambo kwenye tukio hilo la utiani saini makubaliano baina ya pande hizo mbili, lililofanyika kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo.
22
Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakisikiliza kwa kina maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo
3
Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano akizungumza kwenye tukio hilo la utiani saini makubaliano baina ya pande hizo mbili, lililofanyika kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo mchana.
4
Baadhi ya watendaji wa Uchumi na NHC wakifuatilia jambo kwenye hafla hiyo.
5
Baadhi ya watendaji wa NHC wakifuatilia jambo kwenye hafla hiyo.
6
Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakisikiliza kwa kina maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo
7
Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakisikiliza kwa kina maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo
8
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo mchana huu.
9
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo mchana huu.
10
Baadhi ya watendaji wa NHC wakifuatilia jambo kwenye hafla hiyo, Kushoto ni Susan Omari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya, Meneja Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe, Meneja Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Bulla Boma.
11
Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakiwa katika picha ya pamoja.
12
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
13
Watendaji Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) na Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
14
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano na watendaji wake.
15
Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakikata keki kuashiria kuanza kwa ushirikiano endelevu baina ya NHC na USL
16
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
17
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
18
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
19
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
21
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu wakibadilishana hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano
.....................................................................................
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL), leo mchana wametiliana saini makubaliano yatakaziwezesha pande hizo mbili kushirikiana kibiashara ambapo USL itapewa kipaumbele kwenye kupanga katika miradi ya ujenzi ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa popote nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba alisema makubaliano hayo yataziwezesha pande hizo mbili kufaidika na makubaliano hayo.
“Tunachkishuhudia hapa Serena leo ni makubaliano kati ya pande mbili hizi yatakayowezesha kukuza biashara nchini na hivyo kuwafanya Watanzania wengi zaidi kuimarika kiuchumi kwani NHC itafungua fursa kwa uchumi na Uchumi pia watafungua fursa kwa NHC. Miaka ya nyuma kidogo nilipokwenda Kenya nilivutiwa na namna ambavyo Uchumi wanakuza uchumi wa Kenya kwa kununua bidhaa za wakulima wa Kenya, natarajia kile kilichofanyika kule kitafanyika hapa Tanzania pia, kwani ukuaji wa biashara na pesa hauna mipaka,”alisema.
Alisema kwa Uchumi imeweza kutumia fursa hiyo itakayoiwezesha kupata kipaumbele kwenye miradi ya majengo ya biashara popote pale Tanzania na akatoa wito kwa taasisi, mashirika na vyombo vingine kutumia fursa hiyo ili uchumi wan chi uweze kukua.
Naye Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano alisema kuwa Kampuni yake imefurahishwa kuingia katika makubaliano hayo ambayo yataiwesha sasa kupata maeneo bora ya kufanyia biashara kwani wameweza kuingia makubaliano na mwendelezaji nambari moja wa miliki ambaye ataweza kuwapa maeneo mazuri kwajili ya uwekezaji kibiashara.
Alisema watayaenzi makubaliano hayo na hivyo kumudu kukuza uchumi wa Watanzania kwa kuweza kununua bidhaa zao na kuziuza kwenye Supermarkets zao.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo watendaji wa Mamlaka ya ukuzani mitaji na masoko nchini na wadau wengine mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad