KATIBA YETU :SAMUEL SITTA APONGEZWA KWA KULIENDESHA BUNGE MAALUM LA KATIBA KWA UTULIVU NA AMANI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Sept 2014

KATIBA YETU :SAMUEL SITTA APONGEZWA KWA KULIENDESHA BUNGE MAALUM LA KATIBA KWA UTULIVU NA AMANI


 Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusiana na maendeleo ya Bunge hilo wakati alipotembelewa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo na kushoto ni Sheikh Hemed Jalala.
 Baadhi ya Waandishi wakifuatilia mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na mgeni wake Sheikh Hemed Jalala 03 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
 Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akikabidhi kitabu kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (kulia),  kinachoitwa ‘Kilele cha Fasaha’ kinachohusu maadili na uongozi.
 Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akiongoza dua ya kuiombea Bunge Maalum la Katiba. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta na katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Hemed Jalala (wa pili toka kushoto) pamoja ujumbe aliofautana nao. Wa kwanza kulia ni Alhaj Mohamed Mputa, anayemfuatia ni Sheikh Mohamed Abdi na wa tatu toka kulia ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo. Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma
**************************************
Na Magreth Kinabo, Dodoma.
BAADHI ya viongozi wa dini wamempongeza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kwa kitendo chake cha kuliendesha Bunge  hilo vizuri katika hali ya utulivu na amani.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Sheikh Hemed Jalala kutoka Msikiti wa Ghadiir uliopo maeneo ya Kigogo Post jijini Dares Salaam, ambaye aliambatana na Masheikh wengine ambao ni  Alhaji Mohamed Mputa, Sheikh Mohamed Abdi na Masoud Mbilili.

Aidha  Sheikh Jalala akizungumza kwaniaba ya viongozi wenzake wa dini alisema kuwa wamekuja kutembelea Bungeni hapo kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Sitta na kumuunga mkono kwa kazi nzito nzuri anayoifanya huku akisisitiza kuwa wako nyuma yake katika suala hilo.

“Pamoja na changamoto zilizojitokeza umeweza kukabiliananazo vizuri. Sisi na wananchi kila tunapolifuatilia tunaona mmeweza kulipeleka vizuri. Jambo hili ni zito linahitaji amani, utulivu na kuvumiliana,” alisema Sheikh Jalala.

Sheikh Jalala alisema wao kama viongozi wa dini, wameona kuna changamoto ya maadili hivyo, wameandaa kitabu maalum kinachoitwa ‘Kilele cha Fasaha’.

Alisema kitabu hicho kitasaidia kutoa mchango wao kwenye masuala ya uongozi na maadili, ambacho alikikabidhi kwa Mhe. Sitta.

Akipokea kitabu hicho, Mhe.Sitta amesema ni jambo la baraka kwake, ambapo aliahidi kutoa taarifa juu ya jambo hilo na kukikabidhi kitabu hiko katika Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo.

Sheikh Jalala alisema kuna jumla ya nakala 632 ya vitabu hivyo na vimeshakabidhiwa kwenye ofisi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Katika hatua nyingine Sheikh Jalala ameongoza dua maalum kwa ajili ya kuliombea Bunge hilo ili liweze kuendelea kwa amani, utulivu, busara, maelewano na upendo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad