ELIMU NA TEKNOLOJIA :PROGRAMU YA KUFUNDISHA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI YAZINDULIWA DAR ES SALAAM , SEPTEMBA 30-2014 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


1 Oct 2014

ELIMU NA TEKNOLOJIA :PROGRAMU YA KUFUNDISHA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI YAZINDULIWA DAR ES SALAAM , SEPTEMBA 30-2014



  Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akizungumza katika uzinduzi huo. Kampuni ya Tigo, Nokia na Microsoft ndio wadau  mpango huo.
Meneja Mawasiliano wa Microsoft Mobile Devices, Lilian Nganda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na 
Teknolojia Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika 
uzinduzi huo.
 Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
 Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo (katikati), akiangalia simu wakati akiwaelekeza namna ya kutumia simu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania,  Peter Riima (kushoto) na Mrashani Katebeleza, wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
 Hapa uzinduzi huo ukifanyika.
 ' Ni kama anasema' Niacheni nipo kazini nachukua tukio hili nikawahabarishe wengine, chezea mimi nyiee
 Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye 
hafla hiyo ya uzinduzi.
Wadau na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Dotto Mwaibale

WANAFUNZI nchini wametakiwa kutumia mitandao hasa ya simu za mikononi kwa ajili ya kujifunzia masomo mbalimbali badala ya kutumia katika matumizi yasiofaa.

Mwito huo umetolewa na Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki uliofanyika Dar es Salaam leo.

Alisema progamu hiyo imefika wakati muafaka na itawasaidia wanafunzi kujifunza somo hilo muhimu katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

Alisema programu hiyo imeletwa nchini na Kampuni ya Nokia, Tigo kwa kushirikiana na Microsoft,  ambapo serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) inasimamia kwa karibu mpango huo.

Alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika programu hiyo imesaidia kupata mahudhui ya kihisabati jambo litakalo wasaidia wanafunzi kuwa makini kitaaluma.

Alisema matumizi hayo ya simu katika kujifunza hisabati yatakuwa yakifanyika katika muda wa ziada baada ya masomo kwa vile licha ya wanafunzi kumiliki simu lakini hawaruhusiwi kuwa nazo mashuleni.

Mgodo alisema mpango huo kwa sasa upo katika majaribio ukifanikiwa wanaweza kuuingiza katika mitaala ya taifa.

Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska alisema mpango huo umekuwa ukiongeza weredi kwa wanafunzi katika somo la hisabati na ni muhimu katika kipindi hiki cha maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk.Hassan Mshinda alisema tume hiyo ilifanyamchakato na kuukubali mpango huo ambao ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaupungufu mkubwa wa wataalamu wa sayansi wanaotokana na kufaulu kwa somo la hisabati.

"Mradi huu tuliona unafaa kwani utasaidia kuongeza wanasayansi hivyo tuliupokea kwa mikono miwili" alisema Dk.Mshinda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad