MICHEZO YETU : MHE. MEMBE AAHIDI KUENDELEZA DIPLOMASIA YA MICHEZO TANZANIA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Oct 2014

MICHEZO YETU : MHE. MEMBE AAHIDI KUENDELEZA DIPLOMASIA YA MICHEZO TANZANIA




Wanamichezo wakimsikiliza kwa makini Waziri Membe (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.   Viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo wakimsikiliza                   Waziri Membe (hayupo pichani).                     
Wakwanza Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje, Bw.Mkumbwa Ally, na wapili kutoka kushoto ni Afisa Mambo ya Nje Bw. Imani Njalikai wakifuatilia kikao kati ya Waziri Membe na wanamichezo walio shiriki michezo ya jumuiya ya madola Glasgow, Scotland. 
                                      Kikao kikiendele
  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisaini kwenye kitabu cha wageni alipo wasili katika kituo cha Filbert Bayi kilichopo Kibaha Mkuza. 
Katikati ni Mama Bayi akielezea jambo kwa waziri Membe (wa kwanza kulia)  mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, wakwanza kulia ni Bw. Filbert Bayi naye akisikiliza.
Bw. Filbert Bayi akimwonyesha na kumwelezea Waziri Membe Ramani ya eneo lililo na Shule ya awali, msingi, Sekondari na kituo cha michezo cha Filbert Bayi, lililopo Kibaha Mkuza.
Waziri Membe akizungumza alipokuwa akitazama kiwanja cha mpira wa miguu (hakipo pichani), kiwanja hicho cha mpira ni moja kati ya viwanja vinavyotumiwa na wanamichezo waliopo katika kituo hicho cha Filbert Bayi.
Kiwanja cha mpira wa miguu kilichopo katika kituo cha michezo cha Filbert Bayi.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa vyama vya michezo mbalimbali nchini, mara baada ya kumaliza kikao na wanamichezo.Picha na Reginald Philip
          
=========================================
Mhe. Membe Aahidi  Kuendeleza Diplomasia ya Michezo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, amewataka wanamichezo wa Tanzania kutokata tama kwa kufanya vibaya kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka huu, na kuahidi kuendelea kupigania maendeleo ya sekta hiyo.
Akiongea katika kiko cha kutathmini matokeo ya timu ya Tanzania, ambayo haikushinda medali yoyote kwenye michezo hiyo ya Madola, iliyomalizika mjini Glasgow, Scotland mwezi Agosti, Mhe. Membe alisema wizara yake itafanya juhudi zaidi kutafuta wadhamini wa matayarisho ya timu ya taifa ndani na nje ya nchi, chini ya mkakati wa diplomasia ya michezo.
 Kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi wa vyama vya michezo na baadhi ya wanamichezo walioshiriki michezo ya Glasgow, kilifanyika leo kwenye kituo cha michezo cha Filbert Bayi Mkuza.
''Msikatishwe tamaa na matokeo mabaya ya Glasgow, kwani mara nyingi mafanikio huja mara ya pili,'' alisema Mhe. Membe, na kuongeza: ''Tutumie yale yuliyojifunza kwa kushindwa hukokupanga wakati wa ushindi katika mashindano yajayo.''
Mhe. Waziri aliisifu timu ya Tanzania kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu iliposhiriki michezo ya Madola, lakini akasisitiza kuwa nidhamu peke yake haitoshi. ''Nidhamu hiyo ituletee ushindi.'' alisema.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwakushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ilitafuta udhamini wa kambi za mazoezi kwa miezi miwili kwa wanamichezo wa timu ya taifa huko Uturuki, China, Ethiopia, na New Zeland, kabla ya kwenda Glasgow.
Katibu Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Tanzania, Bw. Filbert Bayi, alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo kulichangiwa na muda mfupi wa kukaa kambini na kukosa mashindano ya kujipima nguvu. Ali9shauri idadi ya washiriki na michezo vipunguzwe kulingana na uwezo wa taifa kifedha.
Mkurugenzi wa Michezo, ambaye aliongoza msafara wa Glasgow, Bw. Leornard Thadeo, alisema timu ya Tanzania ilikuwa na ushindani hafifu kutokana na mafunzo hafifu, viwango vya chini vya wachezaji, ukosefu wa vifaa na kuchelewa kutolewa fedha za uwezeshaji.
Walimu wa michezo na wachezaji walisisitiza matayarisho ya muda mrefu zaidi, mazingira mazuri ya mazoezi na udhamini mpana zaidi utakaohusisha taasisi za umma na binafsi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad