MIPANGO YETU :TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


5 Oct 2014

MIPANGO YETU :TUME YA MIPANGO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA JD COMPLEX – KIBAHA, PWANI


Mgeni Rasmi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwantumu Mahiza (aliyesimama) akisisitiza jambo alipokua akifungua kikao cha Baraza hilo.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Rais, Tume ya Mipando kwa pamoja wakiimba wimbo wa Solidarity Forever kuonyesha mshikamano makazini.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakionyesha mshikamano kwa kuimba wimbo wa Solidarity forever mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufungua rasmi kikao hicho.
Kabla ya kuanza majadiliano, wajumbe walimchagua Mwenyekiti Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi ambapo Bibi Magreth Simwela (aliyesimama) aliibuka mshindi kati ya wajumbe watatu waliokua wakigombea nafasi hiyo. Hapo Mwenyekiti Msaidizi alikua akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (Walioketi wa pili kushoto). Walioketi pamoja nae kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bibi Florence Mwanri, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mipango, Bw. Steven Katemba na Katibu wa Baraza Bw. Senya Robert.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad