SIASA ZETU : KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE KWA KISHINDO HUKO ,IRINGA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


12 Oct 2014

SIASA ZETU : KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE KWA KISHINDO HUKO ,IRINGA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata mlo nyumbani kwa Balozi Lucas Mtumbuka (kushoto)wa Shina namba moja eneo la Mkimbizi, alipokwenda kumtembelea yeye na wananchama wake wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Jimbo la Iringa Mjini.
 Kinana akichukua mhogo ambao ni sehemu ya vyakula alivyoandaliwa na balozi
 Kinana akiingia kwenye ukumbi kuzungumza na wanachama 707 wa kikundi cha Iringa Masoko Vicoba ambapo aliahidi kuwasaidia kuipata mkopo mkubwa wa fedha watakazokuwa wanakopeshana.
 Kinana akizungumza na madereva wa daladala baada ya kuzindua tawi la wakareketwa wa CCM, mjini Iringa. Tawi hilo lina wanachama 60.
 Mama Lishe akimnawisha mikono Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambapo yeye na viongozi pamoja na baadhi ya wananchama wa CCM walikwenda kupata chakula cha mchana kwa mama lishe katika Soko Kuu la Iringa .
 Kinana akiapata mlo wa mchana kwa mama lishe mjini Iringa wakati wa mapumziko ya ziara ya kuimarisha uhai wa chama.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Iringa Mjini, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
 Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati (kushoto) akiwa na viongozi wengine wa CCM wakipata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, mjini Iringa.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (katikati) akiwa na viongozi wengine wa CCM wakati wa chakula cha mchana kwa mama lishe.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chongolo, akipata mlo huo wa mchana kwa mama lishe.
 Wanahabari ambao baadhi yao wako kwenye msafara wa Kinana  wakipata mlo wa mchana kwa mama lishe
Kinana akiondoka baada ya kupata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, katika Soko la Iringa Mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihuubia huku mkono wake ukiwa umefungwa POP, katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa, mjini Iringa wa kuhitimisha ziara  ya siku sita mkoani Iringa ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano na wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa, mjini Iringa wa kuhitimisha ziara  ya siku sita mkoani Iringa ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad