Burudani na Maisha : NSSF Yakabidhi Nyumba kwa Wasanii wa Orijino Komedi , Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


7 Nov 2014

Burudani na Maisha : NSSF Yakabidhi Nyumba kwa Wasanii wa Orijino Komedi , Jijini Dar es Salaam


Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni Silvery 'Mpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu)
Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Mac Reagan 'Kipara' na Mjuni Silvery 'Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.
Kushoto, Mac Reagan, Joti na Mpoki wakiangalia nyumba zao walizokabidhiwa na NSSF.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akimkabidhi funguo ya nyumba msanii wa Orijino Komedi.  

Msanii Isaya Mwakilasa 'Wakuvwanga' akipokea funguo ya nyumba yake.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' akipokea funguo ya nyumba yake kutoka kwa Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia)
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa wasanii kikundi cha Orijino Komedi.
Msanii Mac Reagan akizungumza baada ya makabidhiano ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad