Dini Zetu : Mhe. Lowassa Azindua Helikopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima, Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Nov 2014

Dini Zetu : Mhe. Lowassa Azindua Helikopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima, Jijini Dar

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Helkopta itakayotumiwa na Mchungaji huyo katika kazi zake za kiroho,hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na baadhi ya wachungaji waliohudhulia kwenye hafla hiyo.
wakielekea kwenye uzinduzi rasmi wa Helkopta.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Helkopta ya Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kulia kwa Mh. Lowassa).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mtoto wa Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiteta jambo na rubani wa Helkopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.
Helkopta iliyozinduliwa ikipaa kuondoka uwanjani hapo na baadae kurudu mara baada ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakati akimuelezea kuhusu vitabu vyake alivyoviandika kabla ya kuvizindua rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kwenye vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto)
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionyesha moja ya vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto) wakati alipovizindua rasmi .
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam. Picha na Othman Michuzi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad