Mkurugenzi
wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists
Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro akiongoza gari ya Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye
kijiji cha Elang’atadapash wilayani Longido kuzindua mradi mkubwa wa
maji unaofadhiliwa na UNDP.
Na mwandishi wetu
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka
wananchi wa Longido kwa kushirikiana na viongozi wao kutunza vyanzo vya
maji katika wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanafanya maeneo
mengi kuwa makame.
Alvaro
alisema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya
Noondoto na Elang’atadapash uliosaidiwa na UNDP ambao unahudumia wakazi
9,700 na mifugo 47,700.
Mratibu
huyo alisema kwamba utunzaji wa vyanzo vya maji wa mradi huo wenye
thamani ya shilingi milioni 92 utawezesha wanawake kuendelea kushiriki
katika kazi nyingine za jamii badala ya kuhangaika kutwa kusaka maji.
Aidha
alisema viongozi wanatakiwa kuendelea kutoa elimu wa kutunza vyanzo vya
maji na mradi huo ili uwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akiongozana na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la
Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (kulia) mara
baada ya kuwasili katika kijiji cha Elang’atadapash tarafa Kitumbeine
wilaya ya Longido mkoani Arusha kuzindua mradi mkubwa wa maji
uliosaidiwa na UNDP ambao utahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Aliwashukuru
wakazi wa eneo hilo kwa kuthamini na kutambua kwamba mradi huo ni wao
na hivyo kuamini kwamba watafanya kila waliwezalo kuutunza hasa kwa
kuzingatia matatizo yaliyopo sasa ya ukame na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi
huo ambao ulifanyiwa kazi na shirika lisilo la kiserikali la wafugaji
la Ilkisongo Pastoralists initiative,baada ya kupata ruzuku ya UNDP
umelenga kuboresha maisha ya watu, afya ya mifugo na wanyamapori kwa
kuwapatia maji safi na salama.
Aidha
fedha zilizotolewa na UNDP zimefanyakazi ya kujenga tangi la mita za
mraba 45 katika kijiji cha Elang’atadapash,matangi ya kuvuna maji ya
mvua matano na kila moja likiwa na mita za mraba tatu, ukarabati wa
matangi matatu ya kuwezesha msukumo wa maji,kukabarati vituo vya
kuchotea maji vinne na kufundisha vyama vya ushirika vya watumia maji 10
katika kata za Ketumbeine, Elang’atadapash na Iloirienito zilizopo
wilayani Longido.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akisalimiana na wanawake wa Kimasai wa kijiji cha Elang’atadapash
alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji unaofadhiliwa na UNDP.
Aidha wananchi wamefunzwa namna ya kufanya menejimenti ya maji.
Katika
risala yao iliyosomwa na Mike Olemokoro wa Mkurugenzi wa shirika
lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists initiative
IPI Tanzania, wananchi hao pia wamesema mchango wao wa kazi na pia wa
halmashauri katika masuala ya kiufundi yamechukua asilimia 40.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akisalimiana na mmoja wakazi wa kijiji hicho aliyefika kumlaki. Kulia ni
Diwani wa viti maalum kata ya Elang’atadapash wilayani Longido Naini
Mokoro.
Na
hili ndio tangi la mita za mraba 46 katika kijiji cha Elang’atadapash
lililojengwa na UNDP kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama
kwa wakazi wa kijiji hicho ambalo litahudumia wakazi 9,700 na mifugo
47,700.
Mratibu
Kitaifa kutoka UNDP, Bw. Nehemia Mususuri akiteta jambo na Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Katikati
ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo
Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro.
Kikundi cha wakinamama wa Kimasai wakitoa burudani kwa mgeni rasmi kabla ya kuzindua mradi huo wa maji.
Meza kuu.
Mkurugenzi
wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists
Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (mwenye shati jekundi) wakisoma
risala pamoja na mkalimani wa lugha ya Kimasai kwa mgeni rasmi Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Diwani wa viti maalum kata ya Elang’atadapash wilayani Longido Naini
Mokoro, akimvisha kikoi Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez kama shukrani ya jamii ya wafugaji na wakazi wa kata
hiyo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akipokea
fimbo yenye heshima ya uchifu wa kimasai kutoka kwa Diwani wa viti
maalum kata ya Elang’atadapash wilayani Longido Naini Mokoro.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipozi na
baadhi ya wakina mama wa Kimasai wa kijiji cha Elang’atadapash.
Pichani
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akikata utepe kuzindua rasmi mradi mkubwa wa maji wa
kwa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash uliosaidiwa na UNDP. Kushoto
ni Mratibu Kitaifa kutoka UNDP, Bw. Nehemia Mususuri akishuhudia tukio
hilo.
Jiwe la msingi kama linavyosemeka pichani.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika
picha ya pamoja na wakazi wa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash mara
baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez,
akinawa mikono na maji hayo mara baada ya kuzindua rasmi tangi kubwa la
maji kijijini hapo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez,
akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji cha Elang’atadapash, Bi. Nabulu
Kumokndare kama ishara ya kuzindua rasmi mradi huo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez,
akikagua kisima cha maji cha kijiji hicho.
Wanyama
wakinywa maji safi na salama wakati wa sherehe za kuzinduliwa rasmi kwa
mradi mkubwa wa maji utakaohudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mbuzi wakinywa maji kwenye josho maalum litakalotumika kuhudumia mifugo ya vijiji hivyo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez,
akizungumza na wakazi vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash ambapo
aliwaasa kutunza mradi huo kwani maji ni uhai.
Mzee
wa kijiji cha Elang’atadapas, Miaroni Lailuda akimwombea dua na baraka
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez
pamoja na shirika lake kwa msaada huo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez,
akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua mradi huo.
No comments:
Post a Comment