Mazishi : Amigolas Azikwa Katika Makaburi ya Kisutu - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Nov 2014

Mazishi : Amigolas Azikwa Katika Makaburi ya Kisutu



Mwimbaji wa zamani wa bendi ya African Stars, Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki  juzi kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo, anatarajia kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. 

Amigolas alilazwa Hospitali ya Muhimbili siku nne zilizopita kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa na kukutwa na umauti kabla ya kufanyiwa upasuaji. 
Hadi umauti unamkuta Amigolas, alikuwa ni mwimbaji wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 
Amigolas alikuwa mmoja wa wanamuziki waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa uaminifu mkubwa kwa miaka mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na wenzake kadhaa kuanzisha Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na JKT na kuwa Ruvu Stars Band.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad