Muziki na Maisha : Sherehe za Miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma Zafana Sana - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Nov 2014

Muziki na Maisha : Sherehe za Miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma Zafana Sana


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima mpiga solo hodari wa Bendi ya Msondo Ngoma,Abdul Ridhwan "Panga mawe"
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti pamoja fedha taslim sh. Mil. 5,Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) kwa niaba ya baba yake.
Mtangazaji Mkongwe hapa nchini na mwenye historia na Muziki wa Tanzania,Masoud Masoud (kulia) akionyesha moja ya CD za bendi ya Msondo Ngoma zilizokuwa zikinadiwa kwenye sherehe hizo mbele ya Wadhamini.
Safu ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede (katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo.
Abdul Ridhwan "Panga mawe". Picha Zote na Othman Michuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad