Biashara Zetu :Mrisho Gambo Atoa wito kwa Kampuni za Mawasiliano Kusambaza zaidi Huduma zao wilayani kwake - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Dec 2014

Biashara Zetu :Mrisho Gambo Atoa wito kwa Kampuni za Mawasiliano Kusambaza zaidi Huduma zao wilayani kwake

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano  kufungua zaidi  vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Tanga na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo  Korogwe mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.
 Katika kuhakikisha wakazi wa  Korogwe na maeneo jirani   wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita imefungua duka jipya  katika  eneo la Korogwe mjini.
Korogwe ni moja ya kituo maarufu katika  mkoa Tanga ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya  kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.
 Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  eneo hilo na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kaskazini na nchi jirani  kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard   , alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.
“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard
Vodacom ina mtandao wa maduka  86 na wakala mbalimbali wa kuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la pili kufunguliwa katika mkoa wa Tanga.
 Mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini,Maudy Mbaga(kulia)akitoa huduma kwa wateja wa kwanza waliofika katika duka hilo baada ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya hiyo Mrisho Gambo(hayupo pichani)
 Baadhi ya wateja wakipatiwa huduma mbalimbali na mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, Abubakary Lubuva(kushoto)duka hilo lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya hiyo Mrisho Gambo(hayupo pichani)
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo wa kwanza (kulia) akikata utepe kuzinduzua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kulia)akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(kushoto)kuhusiana na kifaa cha Router chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya watu nane kutumia huduma ya intaneti wakati wa uzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu wilaya ya Korogwe mjini.Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu na anaeshuhudia kulia ni Abubakary Lubuva.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad