Habari na Maisha :Kituo cha Redio 5 Chatoa Msaada kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Kihowede , Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Dec 2014

Habari na Maisha :Kituo cha Redio 5 Chatoa Msaada kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Kihowede , Jijini Arusha


SAM_0388Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya “USHINDI”inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
SAM_0393Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono jijini Arusha
SAM_0390Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma
SAM_0363Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
SAM_0376Grace Joseph(12)wa kituo cha kiwohed akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
SAM_0400Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa “NISEME”wimbo wa moto band
SAM_0358Mashindano yakiwa yanaendelea
SAM_0361Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
SAM_0385Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja katika shindano la kucheza muziki
SAM_0346Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
SAM_0352Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
SAM_0350Meneja  ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa Meneja masoko wa Redio 5 Bi.Sarah Keiya
SAM_0366Mtangazaji wa kituo hicho Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
SAM_0405Wafanyakazi wa kituo hicho wakiwa katika maandalizi ya kuwaandalia watoto mapochopocho
SAM_0408Kulia ni mtoto Sharon Nelson akiwa anakabidhi msaada alioleta katika kampeni ya ushindi amewataka watoto wengine kujitolea kusaidia wasionacho
SAM_0371Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
Kampuni Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina “Kampeni ya USHINDI”linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho  Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden. Picha na Pamela Molel wa Jamii Blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad