Hali ya Anga : Tanzania Yaungana na Mataifa Mengine Kuadhimisha Miaka 70 ya Usafiri wa Anga Duniani - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Dec 2014

Hali ya Anga : Tanzania Yaungana na Mataifa Mengine Kuadhimisha Miaka 70 ya Usafiri wa Anga Duniani

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
 Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita akiwahamasisha baadhi ya vijana na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege (hawapo pichani) kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kupata fursa ya kujiunga na fani ya uongozaji wa ndege ndani na nje ya nchi.
 Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita (kulia) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka  namna kitengo cha uongozaji wa ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kinavyofanya kazi na changamoto wanazokabiliana nazo. Kwa Habari Zaidi Bofya Hapa >>>

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad