Happy Birthday : Clouds fm Yasherehekea Kutimiza Miaka 15 Tangu Kuanzishwa Kwake. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Dec 2014

Happy Birthday : Clouds fm Yasherehekea Kutimiza Miaka 15 Tangu Kuanzishwa Kwake.

Mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
Msanii mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
Mkuu wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty.
Dj Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo ya kutimizwa miaka 15 kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na kwingineko.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
Msanii wa zamani wa Bongofleva aliyewahi kuwa kwenye kundi la B Love M,Masiga Msigalla
Kulikuwepo na wimbo wa kuimba pamoja
 Ndafu wa shughuli akiwa mezani
Ndafu akitolewa nje ili aliwe vizuri
Wadau mbalimbali pia walikuwepo.
 Shayo akihakikisha kila mmoja anapata kipande cha Ndafu
 Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akihojiwa machache na Mtangazaji wa Clouds TV,Antonia Nugaz
Kutoka Idara ya Muziki Clouds FM,anaitwa Othman Suka na Da Husna mtangazaji wa kipindi Leo Tena
 Mrope nae akigawa vipande vya Ndafu
Kutabasamu,kuwhatsapika pia kulikwepo mjengoni hapa
''Heee hii imetoka vizuuuriiii..''
 Adam Mchovu akiwatangazia baadhi ya wafanyakazi wenzake kuhusiana na utaraibu mzima wa kwenda kujiachia kwenye kiota cha maraha cha Escape One.
Mazungumzo ya hapa na pale ya kishosti yalinoga pia huku ndafu akiliwa taratibuu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad