Maisha na Matukio : Serikali ya Tanzania Yapiga Marufuku Ujenzi wa Majengo Yasiyo Rafiki na Walemavu - Waziri Lukuvi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Dec 2014

Maisha na Matukio : Serikali ya Tanzania Yapiga Marufuku Ujenzi wa Majengo Yasiyo Rafiki na Walemavu - Waziri Lukuvi

 Waziri  Lukuvi  akimkabidhi  mwanafunzi  wa shule ya Msingi Kipera Rahel Mwikonzi cheti  cha ushiriki mzuri wa siku ya  walemavu
mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa
Kamishina  wa ustawi  wa jamii Bw Dunford Makala akitoa salam zake
Viongozi  mbali mbali  wakiwa pamoja na kamati ya ulinzi  mkoa
Mwenyekiti wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu akiwa na viongozi wa chama cha  walemavu Tanzania kushoto ni makamu mwenyekiti Bi Amina Mollel na katikati ni mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa
Waziri  Lukuvi  akihutubia
Ndumbalo  akipokea  cheti  toka kwa  waziri Lukuvi
Waziri  Lukuvi akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza  (kulia)
Waziri  Lukuvi akimakabidhi cheti  mwanafunzi mlemavu wa shule ya sekondari ya  wasichana Iringa
Katibu wa chama  cha Viziwi Tanzania Bw Shaibu  Juma akiwa katika ulingo wa  wasanii wa ngoma kutoka kikundi cha Viziwi
Walemavu  nchini  wakiwa katika maandamano  leo  wakati wa kilele  cha siku ya  walemavu duniani kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika  mkoa  wa Iringa,kushoto ni mkalimani  wa  kujitolea  ambae ni Mtangazaji wa radio  Nuru Fm Bw  Clement akisaidia  kuwaelekeza  walemavu hao

Hiki  ndicho  cheti  ambacho kampuni ya Asas  imepewa kutokana na ushiriki mzuri wa uchangiaji katika maadhimisho hayo
Waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri  mkuu (sera na uratibu wa bunge) Wiliam Lukuvi akihutubia katika kilele  cha siku ya  walemavu duniani ,maadhimisho  yaliyofanyika katika viwanja vya kichangani mjini Iringa Kitaifa  na Lukuvi kumwakilisha  waziri mkuu Mizengo Pinda
Walemavu  wakiwa katika maadhimisho hayo kitaifa  mjini Iringa
Mwenyekiti wa mkoa  CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu  na mwenyekiti wa UWT  wilaya ya  Iringa mjini wakipongezwa na  waziri  Lukuvi kwa  kuunga mkono maadhimisho ya  siku ya  walemavu nchini
Makamu  mwenyekiti  wa Shivyawata Bi Amina  Mollel akipongezwa na waziri Lukuvi kwa maandalizi mazuri
Walemavu  wakiwa katika maandamano  yao leo
Askari  wa  usalama barabara  Iringa aliyefahamika kwa jina la Sarehe Mollel akiongoza  maandamano ya  watu  wenye  ulemavu  leo   wakati  wa maadhimisho ya siku ya  walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya  kichangani  mjini Iringa na  kuhudhuriwa na waziri wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge Bw  Wiliam Lukuvi kwa niaba ya  waziri mkuu Mizengo Pinda
Waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu  sera  na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akimkabidhi cheti cha ushiriki Tumain  Mdegella kwa  niaba ya ofisi za Neema Crafti mjini Iringa  wakati wa kilele  cha maadhimisho ya  siku ya  walemavu duniani iliyofanyika kitaifa  mjini Iringa
 Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI  imeziagiza  mamlaka  za  usafiri  wa majini na nchi kavu (SUMATRA )  nchini  kuanza mchakato  wa  kukaa na  wamiliki wa  vyombo  hivyo  ili kuanza  uangizaji  wa vyombo  vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni  rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku  majengo ya   serikali kujengwa bila kuwepo kwa  mchoro  unaoonyesha mazingira yanayozingatia makundi  yote ya jamii  likiwemo la walemavu wa viungo .
Agizo   hilo  limetolewa na  waziri  mkuu Mizengo  Pinda wakati  wa maadhimisho ya  siku ya  walemavu  duniani yaliyofanyika   kitaifa  katika  viwanja  vya kichangani mkoani  Iringa jana.
Akiwahutubia   walemavu hao na  wananchi  waliofika katika  viwanja   hivyo waziri  mkuu ,aliyewakilishwa na waziri  wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge)  ,Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa  jimbo la Isimani mkoani Iringa alisema  kuwa  kimekuwepo kilio  cha muda  mwingi  kutoka kwa  walemavu  juu ya kusaulika katika ujenzi  wa  majengo mbali mbali ambayo yamekuwa  yakijengwa  bila kuzingatia  kundi la  watu  wenye  ulemavu jambo ambalo ni sawa na  kuwabagua watu  hao.
Hivyo  alisema  katika  kuona kilio  hicho  cha  walemavu  kinafanyiwa  kazi  kuanzia  sasa majengo  yote ya  serikali  zikiwemo  shule na taasisi nyingine  kabla ya  kuanza  ujenzi  wake lazima  wasimamizi wa  ujenzi  huo kujiridhisha kwa  mchoro ambao  utaonyesha  mazingira  yatakayomuwezesha  mlemavu   kutumia jingo  hilo bila usumbufu  tofauti na  ilivyo sasa ambapo  idadi kubwa ya majengo mazingira  yake  si lafiki kwa  walemavu.
"  Ni  siku  nyingi  watu  wenye ulemavu  wamekuwa  wakilalamika juu ya mazingira  yasiyo rafiki    katika majengo  mbali mbali .....sasa  leo naomba  kuagiza  kuwa michoro yote inayochorwa katika majengo ya  huduma za  kijamii  ni marufuku  kupitishwa ama  wasimamizi  wa  ujenzi  husika  kuruhusu ujenzi  iwapo mchoro hauonyeshi  kama utayajali makundi  yote wakiwemo  walemavu.....wasimamizi  wote msikubali  kusimamia  wala  kutangaza  tenda  ya ujenzi kama ramani  yake  si rafiki kwa  walemavu.....lakini  pia  hata  kwenye mabasi hivi unamtegemea mtu mwenye ulemavu wa miguu ataingia vipi na baiskeli  yake  katika gari iwapo hakuna mazingira  yanayomwezesha  kuingia ....hivi  sasa  teknlojia  imezidi kukua na baadhi ya nchi  wameanza muda mrefu kuwajali walemavu kwa kuwa na mabasi ambayo mlemavu anaingia na baiskeli  yake  na  kushuka nayo   bila usumbufu ni vema hata Sumatra kuangalia uwezekano wa  kuwajali  walemavu hao . pia ni vizuri  hata nyumba  za  ibada  nazo ningeshauri baba askofu   kuangalia kuweka mazingira " alisema  Lukuvi.
Kuhusu  ombi la walemavu hao   hasa  wale  wasio sikia kuomba  serikali  kuwa na wakalimani katika kituo cha Televisheni ya  Taifa (TBC) na vituo  vingine  vya  luninga  ili  kuwawezesha  walemavu hao nao  kuweza  kufuatilia hotuba  ya Rais mwisho  wa mwezi na mambo mengine badala ya  kutengwa ,alisema  kuwa  suala  hilo  ni  wajibu wa  serikali  kuwajali  watu  wake  hivyo tayari  imeuagiza  uongozi  wa TBC na mamlaka ya  mawasiliano Tanzania (TCRA)  kulitafutia  ufumbuzi  suala  hilo la  mkalimani  hasa katika TBC .
Katika  hatua nyingine  Lukuvi  aliwataka  walemavu hao  ili  ombi lao la  kutazamwa katika  nafasi za  uongozi  liweze  kuzingatiwa ni  vema  wao  wenyewe  kujitokeza kwa  wingi  kuipigia  kura  katiba  iliyopendekezwa pindi  itakapokuja kwa  wananchi kwa madai kuwa  katika  katiba   hiyo imezingatia mambo  mengi ya kijamii likiwemo la  kuwajali  watu  wenye ulemavu kwa  kuwatengea nafasi nyingi  zaidi  na  iwapo  katiba  hiyo  itapitishwa kazi ya msuguano wa  rushwa unaweza  kuhamia kwa  walemavu kwa kila mmoja kutaka  kupewa nafasi.
" Hadi  hivi  sasa ni chama cha mapinduzi (CCM) pekee ambacho  kina wabunge wa viti maalum wa  kuteuliwa  kutoka kundi la  walemavu huku  vyama  vingine  vyote  havijawakumbuka kabisa  watu  wenye ulemavu ukiacha  mbunge wa  jimbo la Lindi mjini pekee ambae hakupendelewa  katika ubunge  wake bali alishindwa kihalali kwa  kuchaguliwa na  wananchi  wake..nafikiri  tushirikiane  kuhakikisha katiba  hii iliyopendekezwa  inapita  ili  tuungane pamoja katika  kujenga nchi  yetu "
 Katika  salam  za  walemavu waziri  wa Afya  na ustawi  wa jamii  Dkt Seil S. Rashid  zilizotolewa kwa  niaba  yake  na mwenyekiti  wa baraza la  watu  wenye ulemavu nchini na Dunford Makala   alisema  kuwa  wizara  inaendelea   kuimarisha  ushirikiano na vyama  vya  watu wenye ulemavu  na  shirikiasho  la vyama  vya  watu  wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) katika  kuhakikisha utekelezaji  wa uwekaji  wa fursa  na haki  sawa  kwa  watu  wenye ulemavu nchini .
Alisema  katika  kuhakikisha ushirikiano unakuwepo  wizara yake  imezindua baraza  la  ushauri  la Taifa  la  watu  wenye  ulemavu  toka mnamo 1  Novemba 2014 na katika  hilo  kamwe  hawataacha  kumpongeza  Rais Dkt Jakaya Kikwete  kwa   kumteua  mwenyekiti  wa baraza hilo.
Aidha  alisema  kuwa ni ukweli  usiopingika kuwa nchi  hii chini ya Rais Dkt  Kikwete  imefanya mambo  mengi  zaidi ya  kuwajali  watu  wenye  ulemavu  katika Nyanja  za  kiuchumi ,kiutamaduni na  kisiasa ambavyo  vyote  hivyo  kumwezesha  mlemavu kujikwamua  kimaisha.
Hata   hivyo  alisema  ushahidi  wa yote hayo ni pamoja na kuridhia mikataba  ya kimataifa  juu ya haki  za watu wenye ulemavu , kutungwa kwa sharia Na.9 ya mwaka 2010 ya watu  wenye ulemavu  na kanuni zake ,kuwashirikisha  watu wenye ulemavu  katika tume ya mabadiliko ya katiba  ya Jamhuri ya  muungano wa Tanzania pamoja na kuteuliwa kwa  wajumbe 20  wenye ulemavu  katika  bunge maalumu la mabadiliko ya katiba la mwaka 2014.
Awali  walemavu hao  katika  risala yao  iliyosomwa na makamu  mwenyekiti  wa SHIVYAWATA  Amina Mollel  pamoja na  kuishukuru  serikali kwa jinsi  kwa  kuendelea  kuwa karibu  zaidi na  watu  wenye ulemavu kwa kushiriki shughuli mbali mbali za  walemavu ,bado waliweza  kuishukuru  serikali kwa kuandaa sera ya maendeleo ya  watu wenye ulemavu ya mwaka 2004, kutambuliwa  kwa  watu wenye ulemavu katika MKUKUTA,kuwezesha kuongezeka kwa idadi ya watu wenye ulemavu  wanaopata  elimu kuanzia shule za msingi hadi elimu ya juu na mambo  mengine  mengi ambayo  wao kama  walemavu wamekuwa  wakiona  serikali  yao  ipo pamoja nao.
Sanjari na mema  hayo bado  waliiomba serikali kuzingatia kuwapatia  walemavu mambo muhimu katika maisha ya kila  siku ikiwa ni pamoja na kuwa na vyombo  vya usafiri rafiki kama magari  moshi.vyombo  vya usafiri majini ,angani ,miundo mbinu katika  majengo  na viwanja  vya  ndege ambavyo  vitamwezesha mlemavu pia kuwa  huru.
Mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa maadhimisho hayo yaliyofanyika  chini ya kauli  mbiu  isemayo " Maendeleo endelevu ;Ahadi  ya Teknolojia  huku mkoa  wa  Iringa  ukiendelea  kuwa  bega kwa  bega  na  walemavu ikiwa ni pamoja na  kufanya kazi karibu na  vyama  hivyo  vya  watu  wenye  ulemavu   na kuwa mkoa huo  kwa  sasa una jumla ya  walemavu  zaidi ya 179 ,000 na  wote  serikali  imeendelea  kuwalinda na  kuwa nao pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad