Matukio Kitaifa : Rais Dk. Jakaya Kikwete Amwapisha Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA ,Ikulu Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Dec 2014

Matukio Kitaifa : Rais Dk. Jakaya Kikwete Amwapisha Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA ,Ikulu Dar


Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu Desemba 8, 2014 na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine waandamizi wa serikali.Katikati wapili kushoto anayeshuhudia ni Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gervas Mdemu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa miongozo ya kazi(Standing Orders) Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla ya kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam 
Jumatatu Desemba 8, 2014 
asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla wa kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto Gracious Mathayo Ntebo mjukuu wa wa mkuu mpya wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla ya kumuapisha mkuu huyo wa mkoa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam
Jumatatu Desemba 8, 2014
 . Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad