Matukio : Maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara yafana jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Dec 2014

Matukio : Maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara yafana jijini Dar


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini pamoja na Wananchi wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa jirani wakiwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dare Salaam katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo hufanyika kila mwaka. Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad