Siku ya Ukimwi Duniani :Dk. Gharib Bilal katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani , kitaifa mkoani Njombe - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Dec 2014

Siku ya Ukimwi Duniani :Dk. Gharib Bilal katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani , kitaifa mkoani Njombe


 1:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, kwa pamoja wakisimama kupokea maandamano wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika Desemba 1, 2014 Kitaifa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe, Desemba 1 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka katika uwanja wa Sabasaba baada ya kuhutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa huo Mkoani Njombe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi wakati akiondoka uwanjani hapo baada ya kuhutubia katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, akijumuika na wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Kanisa la KKKT, wakati wakitoa burudani yenye ujumbe kuhusu maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi ya wandamani wakipita mbele ya jukwaa kuu na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu siku ya Ukimwi Duniani wakati wa sherehe hizo zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe Desemba 1, 2014. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad