Uchumi na Biashara : Kagera Kujivunia Uwanja wa Ndege wa Kisasa ,Bukoba Airport. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Dec 2014

Uchumi na Biashara : Kagera Kujivunia Uwanja wa Ndege wa Kisasa ,Bukoba Airport.


Na Saidi Mkabakuli, Kagera

Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.

Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.

“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.

“Kama unavyojionea, sehemu kubwa ya kazi imekamilika, kwa makadirio ni zaidi ya asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanja hiki imeshakamilika,” aliongeza Mhandisi Gobolo.

Kwa mujibu wa mpangokazi wa ujenzi wa kiwanja hicho hadi kufikia mwezi Juni 2014, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami; na ujenzi wa jingo jipya la abiria kufikia hatua ya usimikaji wa paa na mifumo ya maji safi, maji taka na umeme; na kuendelea kwa ujenzi wa jengo la abiria na kituo cha umeme.

Naye, Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amesema kuwa Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa.

“Kwa mujibu Programu ya Matokeo Makubwa Sasa, serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza viwanja vya ndege vyote ili viwe na kiwango kizuri kwa watumiaji wa viwanja hivyo,” alisema Bibi Mwanri.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).
Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.
Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo akitoa maelezo ya namna ya kiwanja hicho kitakavyoonekana mara kitakapokamilika.
Pichani ni muonekano mpya wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Wahandisi Pius Gobolo (kushoto), (Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba) na Suleiman Athuman (watatu kulia), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba wakitoa maelezo mara walipoingia kwenye sehemu ya abiria ya jengo jipya la kiwanja hicho.
Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia) akifafanua jambo kwa Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia ni Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Wapili kushoto) na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo (Kushoto).
Hadi kuleeee.. Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Mbele) akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) sehemu inayopendekezwa kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipangoimu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiendelea na kazi ya ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba. PICHA NA SAIDI MKABAKULI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad