Uchumi Wetu :NMB kutoa Kadi Milioni 1.5 za Malipo za MasterCard nchini Tanzania - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


8 Dec 2014

Uchumi Wetu :NMB kutoa Kadi Milioni 1.5 za Malipo za MasterCard nchini Tanzania


Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Bw.Mark Weissing akiongea na wana habari kuhusu makubaliano kati ya NMB na Master Card katika hafla fupi ya kuweka saini makubaliano hayo.
Daniel Monehin, Rais wa Kitengo, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wa MasterCardalisema (kulia) na Bw.Mark Weissing, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB wakieka saini makubaliano.

MasterCard na National Microfinance Bank(NMB), benki kubwa zaidi Tanzania,leo wametangaza makubaliano ya kutoa kadi milioni 1.5 za malipo za MasterCard ambazo zitasaidia katika kupunguza utumiaji wa fedha taslimu na kuongeza ujumuishaji wa masuala ya kifedha kwa kutoa malipo ya kielektroni.

Kama matokeo ya ushirikiano, NMB itatoa chipu salama ya EMV na PinMasterCard ya malipo, kadi za malipo kwa kipindi cha miaka saba ijayo. Kadi itakuwa na teknolojia isiyo na mawasiliano ya MasterCard, na kuonyesha kadi ya malipo isiyo na mawasiliano ya nchini Tanzania hadi sasa.

Teknolojia isiyo ya mawasiliano inawawezesha wateja kufanya malipo kwa haraka, kwa usalama na kwa ufanisi zaidi, na ni bora kwa mazingira ya malipo ya haraka ambapo kasi na ufanisi huhitajika zaidi kama vile katika kodi, mabasi, wafanyabiashara wakubwa wa rejareja, baa na vituo vya mafuta.

“Benki ya NMB imejitolea kutoa masuluhisho na huduma za kibenki kwa watu binafsi na 
pia
 wafanyabiashara wadogowadogo na wa kati ,” alisema Mark Weissing, Ofisa Mtendaji Mkuu wa National Microfinance Bank . “tunafurahi kufanya kazi pamoja na MasterCard, ambao teknolojia yao ya malipo duniani na utaalamu wao utatoa bidhaa zinazofaa za malipo kwa wateja wetu wanaoongezeka.”

Akitoa maoni yake juu ya ushirikiano , Daniel Monehin, Rais wa Kitengo , Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wa MasterCard alisema:“Kupitia ushirikiano huu , tumeunganisha teknolojia ya malipo ya kimataifa ya MasterCard na mtandao wa matawi na Mashine za ATM wa NMB ili kuwapatia wateja njia ya malipo ambayo inafaa zaidi, salama na ya kuaminika. Ni kwa njia ya ushirikiano kama huu ambapo wananchi wa Tanzania watapata huduma bora zaidi za kifedha na kuweza kufanya miamala kielektoni katika namna ambazo hapo mwanzo hawakuwa wakizifahamu.”

Wateja wenye kadi za NMB wataweza kutumia kadi zao za malipo za MasterCard kutoa fedha kutoka kwenye mashine zaidi ya 600 za NMB nchini Tanzania na kwa mara ya kwanza, kwenye mamilioni ya ATM ambazo zinatumia MasterCard duniani . Pia wanaweza kulipia bidhaa na huduma kwenye mamilioni ya wanyabiashara wa rejareja, vituo vya mafuta, migahawa, maduka ya mtandao na wafanyabiasahra wengine ambao wanatumia huduma za MasterCard katika nchi zaidi ya 210.

Kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa MasterCard ,“Mkabala wa Kimaendeleo wa Ujumuishaji wa Kifedha - A Progressive Approach to Financial Inclusion”, asilimia 37.8 ya Watanzania wana bidhaa za malipo, na idadi isiyojumuishwa ya wananchi waliokuwa nazo toka mwaka 2009.

“Katika kipindi cha miaka michache, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupanua ujumuishaji wa kifedha na huduma za kifedha . Ni kwa kuungwa mkono na serikali na sera za maendeleo za udhibiti na ushirikiano kama hizi, ambazo zinaisaidia nchi kufikia malengo yake ya asilimia 50% hadi kufikia mwaka 2016 kama yalivyowekwa na Mfumo wa Ujumuishaji wa Kifedha ,” alisema Monehin.

“Kwa kufanya kazi kwa pamoja na serikali, taasisi za kifedha, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, tutaweza kusaidia katika malipo ya kisasa nchiniTanzania, kupunguza matumizi ya fedha taslimu, kuzidisha ujumuishaji wa kifedha na kuwawezesha wateja zaidi kushiriki katika uchumi wa kimataifa.”

Kadri Watanzania wengi zaidi watakavopata bidhaa rasmi za kifedha na kuingia kwenye daraja lililoanzishwa linalokua, haja ya kuanzisha huduma bora zaidi za kibenki na bidhaa na nchi zilizoendelea duniani inaongezeka. Ili kukidhi mahitaji haya, NMB pia itaanzisha kadi za Zawadi za Kimataifa bidhaa bora ya MasterCard , kwa wateja wake matajiri, ambao wengi wao ni wasafiri wa mara kwa mara.

Wenye kadi za Zawadi za Kimataifa wataweza kujifunza suala la mrabaha katika matumizi ya kadi zao, ambazo zinaweza kustahili kusafiri kwa ndege zaidi ya mashirika ya ndege 800 duniani kote, kukodi magari kwenye sehemu maalumu za ukodishaji na kukaa katika hoteli zaidi ya160,000 duniani.  

“Hapa NMB,tunaamini kuwa ni muhimu kufikiria mahitaji wanayotaka wateja wetu, na kuwatuza kwa mrabaha. Tunajitahidi kuwa benki ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha programu hii ya zawadi ambayo itafanya wateja wetu matajiri kupata huduma nyingi zaidi zisizo na gharama ,” alisema Weissing.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad