Kampeni za UKAWA /Dodoma : Dodoma ya Simama kwa Muda ,Mkutano wa Edward Lowassa - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


12 Sept 2015

Kampeni za UKAWA /Dodoma : Dodoma ya Simama kwa Muda ,Mkutano wa Edward Lowassa



Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akinadi sera zake kwa umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini humo Septemba 11, 2015, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma Septemba 11, 2015.


Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa mji wa Dodoma waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Barafu mjini humo, kwa ajili ya kusikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.


Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.
Shangwe za nguvu wakati Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikiwasili uwanjani hapo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alieambatana na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwasili kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa kwenye gari lake la wazi huku umati wa wananchi wa Dodoma ukimsindikiza wakati akitokea kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma Septemba 11, 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad