Matukio :Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro atembelea uwanja wa ndege Kia na kutoa maagizo Mazito - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Nov 2015

Matukio :Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro atembelea uwanja wa ndege Kia na kutoa maagizo Mazito


 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ametembelea uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) kujionea ujenzi wa ya upanuzi wa uwanja na shughuli za uwanja wa ndege Katika kikao cha menejimenti ya kampuni ya uendeshaji uwanja KADCO mkuu wa mkoa amewapongeza uongozi kwa kuongeza ndege zinazotua na kuruka, uwezo wakujiendesha kwa kuwa na mapato mazuri na uwezo wa kudhibiti vitendo haramu vya madawa ya kulevya, usafirishaji nyara za serikali na ugaidi Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa ameagiza yafuatayo yatekelezwe.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla (pichani juu)akizungumza na menejimenti ya Kadco katika uwanja wa ndege kuhusiana na Uwanja huo  usiwe njia ya wapitishaji madawa ya kulevya kwani kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akitembelea Uwanja wa Kia na kuwaambia kuwa uwanja huo usiwe njia ya kutorosha nyara za taifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya taifa na raslimali za taifa.
pia  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ameagiza menejimenti kuutangaza uwanja huo kimataifa ili uvutie wageni zaidi kuja kuona vivutio vya utalii tukivyonavyo na kufanya hivyo ni kuongeza pato la taifa.
Mkuu wa mkoa akiongea na menejimenti ya Kadco leo alipotembelea uwanja wa ndege wa Kia mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad